48 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia: “Miongoni mwa du´aa zake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni pamoja na:

اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بكَ مِن زَوَالِ نِعْمَتِكَ، وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وَفُجَاءَةِ نِقْمَتِكَ، وَجَمِيعِ سَخَطِكَ

“Ee Allaah! Hakika najilinda Kwako kutokana na kuondokewa na neema Yako, kubadilika kwa uzima Wako, adhabu Yako ya ghafla na hasira Yako yote.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii tukufu kuna maombi yafuatayo:

1 – Kujilinda kwa Allaah kutokana na kuondoka kwa neema. Neema ni aina ambayo inakusanya neema za kidini na za kilimwengu. Kinyume chake ni majanga, mitihani, adhabu na mabalaa.

2 – Kujilinda kwa Allaah uzima kutobadilika kwenda katika kinyume chake ambacho ni majanga, mtihani, adhabu na mabalaa.

3 – Kujilinda kwa Allaah kutokana na adhabu Yake ya ghafla. Makusudio ni kushtukizwa kwa jambo. Ni kana kwamba anamuomba Allaah asimuharakishie.

4 – Kujilinda kwa Allaah kutokana na kila kinachomkasirisha. Kwa maana nyingine yale yanayopelekea katika ghadhabu Zake au athari zote za hasira za Allaah.

[1] Muslim (2739).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 54
  • Imechapishwa: 14/10/2025