3 – Hoja tata ya tatu wamesema kuwa Shaykh anawaua waislamu. Hili ni tawi la masuala yaliyo kabla. Wanasema kuwa Shaykh anawaua waislamu na anahalalisha kumwagwa damu na mali zao. Tunasema kuwa si kweli. Masuala haya ni tawi ya yaliyotangulia. Washirikina walikataa kuacha shirki na kuzuia njia ya Allaah. Je, mtu aina hii si haki auawe? Amesema (Ta´ala):

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

“Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala siku ya Mwisho na wala hawaharamishi aliyoyaharamisha Allaah na Mtume Wake na wala hawafuati dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, [piganeni nao] mpaka watoe kodi kwa khiyari na hali ni wenye kunyenyekea. Mayahudi wanasema: “´Uzayr ni mwana wa Allaah na manaswara wanasema: “al-Masiyh ni mwana wa Allaah.” – hayo ni maneno ya kwa midomo yao. Wanaiga maneno ya wale waliokufuru kabla. Allaah awaangamize; ni namna gani wanavyogeuzwa hawa!” (09:29-30)

فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Waueni washirikina popote muwakutapo na wachukueni [mateka] na wazungukeni na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waachilieni huru.” (09:05)

Katika Aayah nyingine imekuja:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

“Wakitubu, wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.” (09:11)

Allaah ametuamrisha kuwapiga vita washirikina tukiwa na uwezo na nguvu za kufanya hivo. Lengo ni ili neno la Allaah liweze kushinda na kutokomeza shirki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) ametuamrisha kuwapiga vita washirikina.

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab aliwapiga vita washirikina tu ambao Allaah ameamrisha kuwapiga vita. Isitoshe jengine ni kwamba sio yeye alianza kuwapiga vita, bali wao ndio walianza kumshambulia, kumkabili na kuzuia watu na kukubali ulingano wake. Watu kama hawa Shaykh awaache wawaangamize watu na waangamize waja na miji ilihali anaweza kupambana nao? Huu ni wajibu uliyowajibishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Amesema (Ta´ala):

وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً

“Piganeni vita na washirikina.” (09:36)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wapigeni vita washirikina.”[1]

Amesema tena:

“Pambaneni katika njia ya Allaah.”[2]

“Wapigeni vita wenye kumkufuru Allaah.”[3]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameamrisha kuwapiga vita makafiri na washirikina kwa sababu wanamuabudu asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Dini ni ya Allaah (´Azza wa Jall). Mwenye kuamini dini isiyokuwa ya Allaah, basi ni wajibu kumpiga vita. Asipokubali haki na kurejea nyuma, basi ni wajibu kumpiga vita. Lau kusingelifanywa hivi Uislamu usingelidhihiri. Uislamu haukudhihiri isipokuwa kwa ulingano na jihaad. Uislamu ulidhihiri kwa kulingania katika dini ya Allaah na kupigana jihaad katika njia ya Allaah. Hili ndilo ambalo Mitume walitumilizwa kwalo.

Shaykh (Rahimahu Allaah) hakumshambulia wala kumuua muislamu yeyote na himdi zote njema ni za Allaah. Aliwaua washirikina na wale wenye kuzuia kukubali haki na wakaandika vitabu vyenye kulingania katika kuyaabudu makaburi na wakati huohuo wanawachochea watu kuendelea kubaki juu ya shirki. Watu sampuli hii ndio ambao ni wajibu kuwapiga vita katika kila zama na kila mahali. Watu kama hawa walipigwa vita na Mitume, wanazuoni, makhaliyfah na watawala wa Kiislamu katika zama mbalimbali. Sio Shaykh mwenyewe ambaye aliwaua watu kama hawa ambao waliendelea kubaki katika shirki na kufuru na wakati huohuo wanataka kulinda ´Aqiydah ya washirikina na kuieneza katika mji. Ni waislamu wepi ambao Shaykh aliwaua? Je, Shaykh alimuua mtu ambaye anamuabudu Allaah peke yake na wala hamshirikishi na chochote? Hata siku moja. Je, Shaykh alipambana na waislamu wenye kumuabudu Allaah, kumpwekesha, wanasimamisha swalah, kutoa zakaah na wameshikamana barabara na dini? Hapana. Kinyume chake watu sampuli hii alikuwa akiwanusuru, akiwapa nguvu na akiwasaidia kushikamana na dini. Ama yule mwenye kufanya ukaidi, akakufuru na kushirikisha, mtu kama huyu sio Shaykh mwenyewe aliyempiga vita. Kila mtawala ambaye ana uwezo wa kuwaua washirikina basi ni wajibu kwake kufanya hivo kutokana na amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ

“Waueni washirikina popote muwakutapo na wachukueni [mateka] na wazungukeni… “

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.” (08:39)

Haya ni maamrisho ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Je, haya ni maamrisho ya Shaykh au ni maamrisho ya Allaah? Ni maamrisho ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina… “

Kwa maana kuwafitinisha watu na kuwazuia na dini.

وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“… na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.” (08:39)

Hili ni kwa sababu Allaah amewaumba viumbe kwa lengo la kumuabudu Yeye:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.” (51:56)

Kwa hiyo mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah, lililo la wajibu kwanza ni kumlingania katika Tawhiyd. Akitekeleza na kurejea, ni vyema, vinginevyo ni wajibu kumpiga vita. Bali kuna baadhi ya wanazuoni wenye kuonelea kuwa jihaad katika njia ya Allaah ni nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kichwa cha mambo ni Uislamu, nguzo yake ni swalah na nundu yake ya juu ni kupambana jihaad katika njia ya Allaah.”[4]

Hii inahusu jihaad katika njia ya Allaah na sio jihaad kwa ajili ya chumo la kidunia, kutaka uongozi au kuwa na utawala juu ya mji. Bali ni jihaad katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall) ili neno la Allaah liweze kuwa juu.

“Yule mwenye kupigana ili neno la Allaah liweze kuwa juu, basi huyo ndio yuko katika njia ya Allaah.”[5]

Shaykh (Rahimahu Allaah) alifanya hivo kwa kufuata Qur-aan na Sunnah na yale waliyoafikiana juu yake waislamu kuhusu kuwapiga vita washirikina ambao wamekataa kukubali na kunyenyekea haki na wakati huohuo wanataka kueneza shirki na kufuru ndani ya mji. Ni watu sampuli hii ndio ambao Shaykh (Rahimahu Allaah) aliwapiga vita. Kusema ya kwamba anawaua waislamu – kama wanavyosema watu hawa – ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakumpiga vita muislamu hata mmoja. Vipi angeliweza kufanya hivo? Hawezi kabisa akamuua muislamu. Mapambano yalikuwa kati ya waislamu na makafiri wanaotaka kubaki kuyashikilia makaburi yao na kumuabudu asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Mtu aina hii ndiye ambaye Shaykh alimlingania na akapigana vita kwa ajili yake. Hakupigana vita kwa ajili ya yale wanayoyasema kwamba anachotaka ni uongozi, mali, kutaka kujulikana na kadhalika. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amejaalia kwa watu sampuli hii watu wenye kuwaraddi mbali na Shaykh. Kuna Ruduud kwa watu hawa mbali na watu wa Najd na watu wa kisiwa cha waarabu. Kuna watu Misri, Sudan, India na kwenginepo wamewaraddi. Ruduud hizo zinapatikana. Vilevile kuna watu ´Iraaq na Shaam wamewaraddi. Wote hawa wamewaraddi watu hawa na vitabu vyao vinajulikana na vipo.

Haki iko wazi na himdi zote njema ni za Allaah. Allaah huweka katika dini Yake mwenye kuinusuru:

وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم

“Mkikengeuka Atabadilisha watu wengineo wasio nyinyi, kisha hawatokuwa kama nyinyi.” (47:38)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ

”Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka dini yake, basi Allaah atawaleta watu [badala yao] Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhilah ya Allaah humpa amtakaye; na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote daima.” (05:54)

Shaykh alilingania katika haya. Hii ndio hoja tata au miongoni mwa hoja zao tata kubwa wanaelekezea ulinganizi wake. Yeye mwenyewe (Rahimahu Allaah) ameiraddi. Hali kadhalika wanafunzi zake na watu wengine kutoka katika miji mbalimbali ya Kiislamu wamewaraddi. Ruduud hizo zinapatikana, zimechapishwa na zimeenea na himdi zote njema ni za Allaah. Lililo juu yenu ni kuziuliza, kuzitilia umuhimu na kuzisoma. Huu ndio mwenendo wa Allaah kwa viumbe Vyake ya kwamba anajaalia haki kuwa na wenye kuinusuru na kuiunga mkono vovyote batili itakavyokuwa. Allaah hujaalia dini hii kuwa na wenye kuinusuru. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakitoacha kikundi katika ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hawatowadhuru wale wenye kuwakosesha nusura wala na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”2

[1] al-Bukhaariy (7095).

[2] Ahmad (02/524) na at-Tirmidhiy (1650) ambaye amesema kuwa Hadiyth ni Hasan.

[3] Muslim (1731), Abu Daawuud (2612) na (2613), at-Tirmidhiy (1408) na (1617), Ibn Maajah (2858), ad-Daarimiy (2444) na (2447) na Ahmad (05/352-358).

[4] Ahmad (05/231), at-Tirmidhiy (2616) na Ibn Maajah (3973).

[5] al-Bukhaariy (281) na Muslim (1904).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 48-56
  • Imechapishwa: 08/02/2026