2 – Hoja tata ya pili wamesema kuwa Shaykh anawakufurisha waislamu. Tunawauliza ni waislamu wepi ambao Shaykh aliwakufurisha? Tubainishieni nao. Ikiwa mnamaanisha kuwa Shaykh amewakufurisha waabudu makaburi, watu hawa wamekufurishwa na Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanazuoni wa waislamu kwa maafikiano. Yule mwenye kumuomba asiyekuwa Allaah, anaabudu asiyekuwa Allaah, anaomba uokozi kwa asiyekuwa Allaah kutoka kwa wafu, anayaomba msaada makaburi na anatoka nje ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), watu sampuli hii sio Shaykh mwenyewe (Rahimahu Allaah) aliyewakufurisha na kuonelea kuwa ni wapotevu. Watu sampuli hii Allaah amewakufurisha ndani ya Qur-aan, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewakufurisha katika Sunnah na wanazuoni kwa maafikiano wamewakufurisha. Mwenye kumuomba asiyekuwa Allaah, akachinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allaah, akamuwekea nadhiri asiyekuwa Allaah, akawaomba msaada wafu, akatufu kwenye makaburi na akawaomba uokozi, huyu ni mshirikina kwa mtazamo wa Shaykh na maimamu wengine. Watu sampuli hii sio Shaykh mwenyewe aliyewakufurisha. Shaykh hakumkufurisha muislamu yeyote mwenye kusema “Laa ilaaha illa Allaah” kwa haki na wakati huohuo anamuabudu Allaah na hamshirikishi Allaah. Shaykh hakumkufurisha muislamu na himdi zote njema ni za Allaah.
Kwa haya madai yao ya kwamba Shaykh anawakufurisha waislamu yatakuwa yamebatilika. Tunawajibu kwa kusema ya kwamba Shaykh anawakufurisha washirikina tu. Vitabu vyake vinapatikana. Ruduud zake zinajulikana. Maneno yake yameandikwa; kwamba Shaykh hakumkufurisha yeyote isipokuwa yule aliyekufurishwa na Allaah katika Qur-aan, yule aliyekufurishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Sunnah au yule ambaye wanazuoni wameafikiana juu ya kumkufurisha. Nao si wengine ni wale wenye kujenga majengo kwenye makaburi na wanayaabudu badala ya Allaah. Wakifanya hivo kwa kuwaiga Laat, ´Uzzaa na Manaat mwengine watatu. Wanaiga masanamu yaliyokuwepo kabla ya kuja Uislamu. Amesema (Jalla wa ´Alaa):
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
“Na wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao [hawawezi] kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah. Sema: “Je, mnamjulisha Allaah kwa yale asiyoyajua katika mbingu na ardhini?” Utakasifu ni Wake na ametukuka juu kabisa kutokamana na yale yote wanayomshirikisha.” (10:18)
Ameita wayafanyayo kuwa ni shirki na Akajitakasa Mwenyewe kutokana nayo ilihali wao wanasema kuwa ni waombezi. Vivyo hivyo ndivyo wanavofanya waabudu makaburi hii leo. Wanasema kuwa wanataka kutoka kwao uombezi wawaombee kwa Allaah. Wanawachinjia na wanawaomba uokozi na kusema ya kwamba wanajua kuwa hawamiliki kitu, lakini wanachotaka tu ni wawaombee. Haya haya ndio yaliyosemwa na washirikina wa hapo kabla. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):
أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ ۚ وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ
“Tanabahi! Ni ya Alllaah pekee dini iliyotakasika. Na wale wanaowafanya wengine badala Yake kuwa walinzi [wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” Hakika Allaah atahukumu baina yao katika yale yote waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah hamwongoi aliye muongo, kafiri.” (39:03)
Amewakadhibisha na kuwakufurisha na wao huku wanasema ya kwamba hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu. Wamekubali wenyewe kuwa wanawaabudu. Hivi kweli mtu anayemuabudu asiyekuwa Allaah ni muislamu? Wao wenyewe wamekubali na kusema ya kwamba hatuwaabudu. Wamekubali kuwa wanawaabudu. Mwenye kumuabudu asiyekuwa Allaah ni kafiri. Hili ndio alilosema Shaykh na wanazuoni wengine wa Kiislamu. Himdi zote njema ni za Allaah kuona hakuwakufurisha waislamu. Aliwakufurisha washirikina tu ambao wanamuabudu asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall); wanachinjia, wanaweka nadhiri, wanatufu na kuwaomba uokozi wafu. Shaykh alikufurisha watu sampuli hii na sio yeye mwenyewe aliyefanya hivo (Rahimahu Allaah). Badala yake alilingania katika yale aliyolingania Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kulingania katika Tawhiyd na kukemea shirki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا
“Mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote.” (04:36)
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ
“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.” (21:25)
Haya ndio aliyolingania Shaykh: kumuabudu Allaah peke yake na kukataza kumuabudu asiyekuwa Yeye. Hii ndio maana ya “Laa ilaaha illa Allaah”. Maana yake ni ukanushaji na uthibitishaji. Ndani yake mna kukanusha shirki na kuthibitisha Tawhiyd. Je, hii si ndio maana ya “Laa ilaaha illa Allaah”. Huu ndio ulinganizi wa Shaykh ambapo ilikuwa ni kukemea shirki na kuamrisha Tawhiyd. Je, huku ni kuwakufurisha waislamu? Ni kuwakufurisha makafiri ambao wanamuabudu asiye Allaah (´Azza wa Jall).
Leo hii wanapatikana na haya ndio matendo yao juu ya makaburi. Vipi watajikana ilihali wanayofanya leo ni yale yale waliyokuwa wakifanya watu kabla ya kuja Uislamu katika wakati wa Abu Lahab na Abu Jahl. Wanaabudu asiyekuwa Allaah kama walivyokuwa wakifanya watu kabla ya kuja Uislamu. Bali wao ni wabaya zaidi kuliko waliyokuwa wakifanya watu kabla ya kuja Uislamu. Ametakasika Allaah kutokana na mapungufu. Wanasema kuwa tunawakufurisha ilihali wanamuabudu asiyekuwa Allaah. Je, yule anayemuabudu asiyekuwa Allaah ni kafiri au muislamu? Kila mtu atajibu kwa kusema kuwa ni kafiri na ni mshirikina.
Ulinganizi wa Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ndio ulinganizi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na pia ndio ulinganizi ya wanazuoni waliokuja baada yake. Hakulingania katika kitu kinachotoka nje ya ulinganizi wa Mitume. Ulinganizi wake ulikuwa ni wa kulingania katika Tawhiyd na kukataza shirki.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 40-48
- Imechapishwa: 08/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 40-48
Imechapishwa: 08/02/2026
https://firqatunnajia.com/09-ibn-abdil-wahhaab-anawakufurisha-waislamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket