Swali 7: Je, msemo huu ni sahihi:
“Yeyote anayesema kuwa imani ni maneno, matendo na kuamini, huongezeka na kupungua, basi amejitenga kabisa na madhehebu ya Murji-ah, hata ikiwa atasema kuwa hakuna ukafiri isipokuwa kwa kuitakidi na kukanusha”?
Jibu: Sentesi ya mwisho inachengua sentesi ya kwanza. Maneno yake:
“Yeyote anayesema kuwa imani ni maneno, matendo na kuamini, huongezeka na kupungua.”
ni haki na ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa’ah. Lakini maneno yake baada ya hayo:
”… hakuna ukafiri isipokuwa kwa kuitakidi na kukanusha.”
yanachengua jumla ya kwanza. Kama ambavyo imani inakuwa kwa maneno, matendo na kuamini, vivyo hivyo ukafiri unakuwa kwa maneno, matendo na kuamini. Hivyo basi inapaswa kusahihisha jumla ya pili na iwe namna ifuatayo:
“Ukafiri pia unakuwa kwa maneno, matendo na imani.”
Lakini msemo huu kubaki kama ulivyo itambulike kuwa sehemu ya mwisho inachengua sentesi ya kwanza.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 24
- Imechapishwa: 01/01/2026
Swali 7: Je, msemo huu ni sahihi:
“Yeyote anayesema kuwa imani ni maneno, matendo na kuamini, huongezeka na kupungua, basi amejitenga kabisa na madhehebu ya Murji-ah, hata ikiwa atasema kuwa hakuna ukafiri isipokuwa kwa kuitakidi na kukanusha”?
Jibu: Sentesi ya mwisho inachengua sentesi ya kwanza. Maneno yake:
“Yeyote anayesema kuwa imani ni maneno, matendo na kuamini, huongezeka na kupungua.”
ni haki na ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa’ah. Lakini maneno yake baada ya hayo:
”… hakuna ukafiri isipokuwa kwa kuitakidi na kukanusha.”
yanachengua jumla ya kwanza. Kama ambavyo imani inakuwa kwa maneno, matendo na kuamini, vivyo hivyo ukafiri unakuwa kwa maneno, matendo na kuamini. Hivyo basi inapaswa kusahihisha jumla ya pili na iwe namna ifuatayo:
“Ukafiri pia unakuwa kwa maneno, matendo na imani.”
Lakini msemo huu kubaki kama ulivyo itambulike kuwa sehemu ya mwisho inachengua sentesi ya kwanza.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 24
Imechapishwa: 01/01/2026
https://firqatunnajia.com/07-msemo-hakuna-ukafiri-isipokuwa-kwa-kuitakidi-na-kukanusha/