Hali kadhalika inahusiana na Mitume. Ni wajibu kuwaamini kwa jumla na kwa upambanuzi. Tunatakiwa kuamini kuwa Allaah (Subhaanah) amewatumia waja Wake Mitume wenye kutoa bishara njema na maonyo na wanaolingania katika haki. Atayewaitikia, basi huyo amefuzu kwa furaha, na atayewakhalifu huyo amekula khasara na majuto. Mtume wa mwisho na ambaye ni bora ni Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Subhaanah) amesema:
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Hakika tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ
“Mitume ambao ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya Mitume [hao kuletwa].” (04:165)
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ
“Muhammad hakuwa ni baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.” (33:40)
Wale waliotajwa na Allaah au wamethibiti kutajwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi tunatakiwa kumuamini kwa njia ya upambanuzi na kwa dhati zao kama mfano wa Nuuh, Huud, Swaalih, Ibraahiym na wengineo (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 09
- Imechapishwa: 30/05/2023
Hali kadhalika inahusiana na Mitume. Ni wajibu kuwaamini kwa jumla na kwa upambanuzi. Tunatakiwa kuamini kuwa Allaah (Subhaanah) amewatumia waja Wake Mitume wenye kutoa bishara njema na maonyo na wanaolingania katika haki. Atayewaitikia, basi huyo amefuzu kwa furaha, na atayewakhalifu huyo amekula khasara na majuto. Mtume wa mwisho na ambaye ni bora ni Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Subhaanah) amesema:
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Hakika tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuut [miungu ya uongo].”” (16:36)
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ
“Mitume ambao ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya Mitume [hao kuletwa].” (04:165)
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ
“Muhammad hakuwa ni baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.” (33:40)
Wale waliotajwa na Allaah au wamethibiti kutajwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi tunatakiwa kumuamini kwa njia ya upambanuzi na kwa dhati zao kama mfano wa Nuuh, Huud, Swaalih, Ibraahiym na wengineo (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 09
Imechapishwa: 30/05/2023
https://firqatunnajia.com/07-kuwaamini-mitume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)