3 – Kuhusiana na Hadiyth ya Abu Muusa al-Ash‘ariy, ameipokea Ibn Maajah (560). Wameitia kasoro kwa sababu mbili:
1 – Mpokezi wake ‘Iysaa bin Sinaan al-Hanafiy al-Filistwiyniy amedhoofishwa na Ahmad, Ibn Ma‘iyn na wengineo.
Lakini Ibn Hibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat”. Basi mtu wa aina hii udhaifu wake unavumilika na Hadiyth yake huwa karibu zaidi na uzuri kuliko udhaifu, khaswa kwa ukiziungatia pia kwamba al-Bukhaariy ameinyamazia Hadiyth hii. Lau ingekuwa dhaifu kwake basi angebainisha hilo, kama itakavyokuja huko mbele.
2 – Taabi‘iy, ambaye ni adh-Dhwahhaak bin ‘Uthmaan bin ‘Arzab, anayepokea kutoka kwa Abu Muusa lakini hakusikia kutoka kwa Abu Muusa.
Hili ni dai pana. Limetajwa na Ibn Abiy Haatim kutoka kwa baba yake katika wasifu wa adh-Dhwahhaak, ambaye amesema:
”Sahihi zaidi ni kwamba amepokea kutoka kwa Abu Muusa ikiwa na cheni ambayo kuna Swahabah anayekosekana.”[1]
Lakini al-Bukhaariy – naye ndiye hoja katika jambo hili – amemtaja na akasema:
”Amemsikia Abu Muusa.”[2]
Kisha akaashiria Hadiyth hii katika wasifu wake kwa ishara fupi kama ilivyo desturi yake. Akamnyamazia wala hakumtaja kasoro yoyote. Hivyo ikabainika kuwa angalau kwa uchache ni Hadiyth inayokubalika.
[1] al-Jarh wat-Ta´diyl (2027).
[2] at-Taariykh al-Kabiyr (2/2/334).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 11-12
- Imechapishwa: 01/04/2026
3 – Kuhusiana na Hadiyth ya Abu Muusa al-Ash‘ariy, ameipokea Ibn Maajah (560). Wameitia kasoro kwa sababu mbili:
1 – Mpokezi wake ‘Iysaa bin Sinaan al-Hanafiy al-Filistwiyniy amedhoofishwa na Ahmad, Ibn Ma‘iyn na wengineo.
Lakini Ibn Hibbaan amemtaja katika ”ath-Thiqaat”. Basi mtu wa aina hii udhaifu wake unavumilika na Hadiyth yake huwa karibu zaidi na uzuri kuliko udhaifu, khaswa kwa ukiziungatia pia kwamba al-Bukhaariy ameinyamazia Hadiyth hii. Lau ingekuwa dhaifu kwake basi angebainisha hilo, kama itakavyokuja huko mbele.
2 – Taabi‘iy, ambaye ni adh-Dhwahhaak bin ‘Uthmaan bin ‘Arzab, anayepokea kutoka kwa Abu Muusa lakini hakusikia kutoka kwa Abu Muusa.
Hili ni dai pana. Limetajwa na Ibn Abiy Haatim kutoka kwa baba yake katika wasifu wa adh-Dhwahhaak, ambaye amesema:
”Sahihi zaidi ni kwamba amepokea kutoka kwa Abu Muusa ikiwa na cheni ambayo kuna Swahabah anayekosekana.”[1]
Lakini al-Bukhaariy – naye ndiye hoja katika jambo hili – amemtaja na akasema:
”Amemsikia Abu Muusa.”[2]
Kisha akaashiria Hadiyth hii katika wasifu wake kwa ishara fupi kama ilivyo desturi yake. Akamnyamazia wala hakumtaja kasoro yoyote. Hivyo ikabainika kuwa angalau kwa uchache ni Hadiyth inayokubalika.
[1] al-Jarh wat-Ta´diyl (2027).
[2] at-Taariykh al-Kabiyr (2/2/334).
Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 11-12
Imechapishwa: 01/04/2026
https://firqatunnajia.com/07-hadiyth-ya-abu-muusa-kuhusu-kupangusa-juu-ya-soksi-angalau-kwa-uchache-ni-yenye-kukubaliwa/