07. Hadiyth ”Nilimwona Mtume wa Allaah akiswali akiwa na viatu… ”

Abu Daawuud (1/247-248) amesema: Muslim bin Ibraahiym ametuhadithia: ´Aliy bin al-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa Husayn al-Mu´allim, kutoka kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza:

”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali akiwa na viatu na akiwa peku.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah (1/330), Ahmad (2/174, 178, 179, 190 na 215), Ibn Abiy Shaybah (2/415), Ibn Sa´d (2/168 – mswada), at-Twahaawiy (1/512) na al-Bayhaqiy (1/421). Hadiyth ni nzuri[2].

[1] Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa  al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (653).

[2] Ikiwa cheni ya wapokezi imesihi hadi kwa ´Amr bin Shu´ayb, kama ilivyo katika hali hii, basi Hadiyth hiyo ni nzuri.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 10
  • Imechapishwa: 28/05/2025