46 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika du´aa yake:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ، وَشَرِّ مَا لَمْ أَعْمَلْ
“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na shari niliyofanya na shari ambayo sikufanya.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Najilinda Kwako kutokana na shari niliyofanya na shari ambayo sikufanya katika matendo ambayo kuyaacha kwake inakuwa ni sababu ya kuangamia na kupata ghadhabu. Kuna uwezekano vilevile anakusudia uovu wa matendo ya watenda madambi wengine, kwa sababu adhabu yake ni yenye kuwaenea wengine pia. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً
“Na ogopeni fitina ambayo haitowasibu pekee wale waliodhulumu [nafsi zao] miongoni mwenu.”[2]
Du´aa hii ni tukufu. Imekuja katika upokezi wa an-Nasaa´iy ya kwamba ilikuwa ndio du´aa anayoomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wingi[3].
[1] Muslim (2716).
[2] 08:25
[3] an-Nasaa´iy (5524).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 52
- Imechapishwa: 14/10/2025
46 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema katika du´aa yake:
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا عَمِلْتُ، وَشَرِّ مَا لَمْ أَعْمَلْ
“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na shari niliyofanya na shari ambayo sikufanya.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Najilinda Kwako kutokana na shari niliyofanya na shari ambayo sikufanya katika matendo ambayo kuyaacha kwake inakuwa ni sababu ya kuangamia na kupata ghadhabu. Kuna uwezekano vilevile anakusudia uovu wa matendo ya watenda madambi wengine, kwa sababu adhabu yake ni yenye kuwaenea wengine pia. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً
“Na ogopeni fitina ambayo haitowasibu pekee wale waliodhulumu [nafsi zao] miongoni mwenu.”[2]
Du´aa hii ni tukufu. Imekuja katika upokezi wa an-Nasaa´iy ya kwamba ilikuwa ndio du´aa anayoomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wingi[3].
[1] Muslim (2716).
[2] 08:25
[3] an-Nasaa´iy (5524).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 52
Imechapishwa: 14/10/2025
https://firqatunnajia.com/07-duaa-ya-kujilinda-kwa-allaah-na-shari-ya-uliyofanya-na-ambayo-hukufanya/