Baadhi ya waliokuja nyuma wanasema kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya mfumo wa Salaf na mfumo wa Mu´awwilah. Wanamaanisha kuwa mifumo yote miwili ni yenye kuafikiana juu ya kwamba Aayah na Hadiyth hazifahamishi juu ya sifa za Allaah. Tofauti pekee ni kuwa Mu´awwilah wanaonelea kuwa kuna haja ya kuzifasiri na kuziteulia maana/makusudio yake. Kuhusiana na Salaf, waliacha kuziteulia maana kwa uwezekano wa kwamba maandiko yanaweza kuwa na maana nyengine.
Huu ni uongo wa wazi kwa Salaf. Hakuna yeyote katika wao aliyekanusha ile dalili yenye kufahamishwa na sifa za Allaah inayolingana Naye pekee. Bali maneno yao yanafahamisha kuthibitisha sifa kwa jumla na kuwakemea wale wenye kuzikanusha au kumshabihisha Allaah na viumbe Wake. Kwa mfano amesema Nu´aym bin Hammad al-Khazaa´iy, ambaye ni mwalimu wa al-Bukhaariy:
“Yule mwenye kumshabihisha Allaah na viumbe Wake amekufuru. Mwenye kukanusha kitu katika yale Allaah amejisifia Mwenyewe amekufuru. Hata hivyo haizingatiwi kuwa ni kushabihisha kumthibitishia Allaah yale aliyojithibitishia Mwenyewe na yale ambayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemthibitishia.”[1]
Salaf wana maneno mengi katika jambo hili.
Kinachoonyesha kuwa Salaf walikuwa ni wenye kuthibitisha sifa na kwamba hawakuwa wakiafikiana kabisa na Mu´awwilah, ni kwamba Mu´awwilah walikuwa ni maadui zao. Walikuwa wakiwatuhumu kumshabihisha Allaah na viumbe na kumfanya kuwa na kiwiliwili kwa sababu tu wamethibitisha sifa. Lau kweli Salaf walikuwa wakiafikiana nao kwamba maandiko hayafahamishi juu ya sifa za Allaah, basi wasingelikuwa maadui zao au kuwatuhumu kwamba wanamshabihisha Allaah na viumbe na kumfanya kuwa na kiwiliwili. Hili ni jambo liko wazi kabisa na himdi zote ni za Allaah.
[1] adh-Dhahabiy katika ”Siyar” (01/610). Katika (13/299) amesema:
”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh zaidi.”
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 33
- Imechapishwa: 09/01/2020

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 33
Imechapishwa: 09/01/2020
https://firqatunnajia.com/07-baadhi-ya-waliokuja-nyuma-wanaivisha-haki-batili-2/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)