6- Wanawashambulia, kwa siri na kwa dhahiri, watawala na wanachuoni ikiwa ni pamoja vilevile na Muftiy wa ulimwengu wa Kiislamu ambaye fadhila zake, elimu yake, kuipa kwake nyongo dunia na uchaji Allaah umethibitishwa hata na maadui wa Uislamu. Lakini anakosolewa na al-Ikhwaan al-Muslimuun kwa njia ambayo waandishi wa kawaida hawawezi kufanya. Nilisikiza mkanda ambapo mwanaharakati mmoja katika kisiwa cha Kiarabu anamzungumzisha Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) akisema yafuatayo:
Na wewe, ambaye unasifiwa kwa utukufu na ukarimu
umekuwa pamoja na dini ya wenye kutukanywa
Niwaambie nini Ummah na vijana?
Niseme nini ilihali wewe mwenyewe umesibiwa?
Umekuja kama kamanda wa farasi na wapandaji wao
ili mumuue mwalimu wangu juu ya minbari yangu[1]
[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:
“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 19
- Imechapishwa: 25/03/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)