´Allaamah al-Mubaarakfuuriy (Rahimahu Allaah) alijitwisha taabu kubwa katika kuidhoofisha Hadiyth hii, jambo ambalo kwa mtu mlinganifu mwenye uadilifu na uchunguzi anaiona kuwa si sahihi. Miongoni mwa mambo ya kushangaza zaidi aliyoyafanya ni kumjibu yule aliyesema kwamba riwaya ya Huzayl ni ongezeko kutoka kwa mtu mwenye kuaminika na hivyo inakubalika, akasema:
”Hili ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Kwa sababu watu wote wamepokea kutoka kwa al-Mughiyrah kwa tamko lisemalo: ”Alipaka juu ya soksi za ngozi.” Abu Qays amewapinga wote kwa kupokea kutoka kwa Huzayl, kutoka kwa al-Mughiyrah kwa tamko lisemalo: ”Alipaka juu ya soksi za kawaida na viatu.” Basi hakuzidisha juu ya walichokipokea, bali amepinga walichokipokea. Ni kweli kwamba kama angepokea kwa tamko lisemalo: ”Alipaka juu ya soksi za ngozi, soksi za kawaida na viatu”, ndipo ingesemwa kwamba amepokea jambo la ziada.”[1]
Hivyo ndivyo alivyosema, jambo ambalo ni kubadilisha mtazamo. Kwa sababu kusudi si kwamba amepokea ziada katika tamko la Hadiyth, bali waliokusudia kusema ni ziada wamelenga kwamba amepokea hukumu nyingine ya ziada juu ya walichokipokea wengine. Wao wamepokea kupaka juu ya soksi za ngozi, naye amepokea kupaka juu ya soksi za kawaida. Wala hakukanusha riwaya ya kupaka juu ya soksi za ngozi. Riwaya yake kwa hakika ni ziada juu ya riwaya za wengine. Hili liko wazi kwamba hukumu ya kuwatia makosa wapokezi wenye kuaminika katika riwaya ya Hadiyth hii ni hukumu isiyo na dalili, kama tulivyobainisha. Isitoshe upokezi wake umeungwa mkono kwa matendo ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ambao Ibn-ul-Qayyim mwenyewe amesimulia hoja ya kutegemea matendo yao. Kwa hiyo hakupokea hukumu ya ajabu inayopingana na ambayo hakuna yeyote aliyeisema, bali alipokea tendo ambalo imethibiti kuwa Maswahabah hao walilitenda na wakafanyia kazi hukumu yake.
[1] Tuhfat-ul-Ahwadhiy (1/100-102).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 10-11
- Imechapishwa: 01/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 10-11
Imechapishwa: 01/04/2026
https://firqatunnajia.com/06-taabu-kubwa-ya-al-mubaarakfuuriy-katika-kuidhoofisha-hadiyth-ya-al-mughiyrah/