Maadui wa Tawhiyd walipingana na ulingano wa Shaykh. Watu hawa walipingana na Shaykh kwa hoja tata mbalimbali, jambo ambalo sio jipya. Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) walipingwa. Amesema (Jalla wa ´Alaa):
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ
”Namna hiyo ndivyo Tulivyofanya kwa kila Nabii maadui mashaytwaan wa kiwatu na kijini – wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya kudanganya. Lau angetaka Mola wako wasingeliyafanya hayo; basi waachilie mbali na wanayoyazusha.” (06:112)
Haina maana kuwa watu hawa wanazungumza maneno ya kawaida. Bali wanazungumza maneno mbayo yaliopambwapambwa yanawadhuru watu madhaifu wasiokuwa wasomi. Hawa ndio hutiwa mchanga wa machoni. Ni maneno yaliopambwapambwa, yenye kutatiza na yaliyorembwa. Lakini hata hivyo ni maneno batili. Haijalishi kitu batili namna itakavyopambwa na kurembwa itabaki kuwa ni batili na hainufaishi kitu.
يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا
”Wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya kudanganya.”
Ni maneno ya udanganyifu kwa ajili ya kuwapa mtihani na majaribio watu. Haya ndio yalimfika Shaykh (Rahimahu Allaah). Ana kiigizo kwa wajumbe, wanazuoni na watengenezaji wengine waliomtangulia. Kulisemwa nini juu ya Imaam Ahmad? Kulisemwa nini juu ya Abu Haniyfah, Ahmad, Maalik na ash-Shaafi´iy? Sivyo tu, bali kulisemwa nini juu ya Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kulisemwa nini juu ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na maimamu wengine watengenezaji? Kulisemwa na kufanywa mengi. Hili sio jambo maalum kwa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Huu ni mwenendo wa Allaah kwa viumbe Wake ambapo anawapa mtihani waja Wake. Allaah anawapa mtihani kwa watu sampuli hii ambao wanalingania katika upotevu. Watu hawa wanakuwa bega kwa bega na wale wanaolingania katika haki.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 29-31
- Imechapishwa: 07/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 29-31
Imechapishwa: 07/02/2026
https://firqatunnajia.com/06-ibn-abdil-wahhaab-si-wa-kwanza/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket