Hadiyth ya nne

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?”[1]

وَفِي السَّمَاء رازِقُكُم وَمَا تُوعَدُونَ

“Juu ya mbingu Yuko Mruzuku wenu na yale mnayoahidiwa.”[2]

Ibn Muhayswin alisoma namna hiyo.

يَا عِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”[3]

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

”Bali Allaah alimnyanyua Kwake. Allaah ni Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye hekima wa yote.”[4]

2 – Ahmad bin Salaamah al-Muqriy’ ametukhabarisha kwa maandishi, kutoka kwa Mas´uud bin Abiy Mansuur al-Jammaal: Ghaanim al-Burjiy ametuhadithia mwaka wa 508 na mimi nikiwepo: Abu Nu´aym al-Haafidhw ametuhadithia: Habiyb bin al-Hasan ametuhadithia, ´Umar bin Hafsw as-Saduusiy ametuhadithia: ´Aaswim bin ´Aliy ametuhadithia: Ibn Abiy Dhi’b ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr bin ´Atwaa’, kutoka kwa Sa´iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati mtu anapokufa ikiwa mtu alikuwa mwema anajiwa na Malaika ambao wanasema: “Toka, ee nafsi nzuri iliokuwa kwenye mwili mzuri. Toka ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Kutaendelea kusemwa hivo mpaka pale inapotoka. Halafu ipandishwe juu mbinguni. Itaombewa idhini ya kuingia ambapo kutasemwa: “Ni nani huyu?” Kutasemwa kwamba ni fulani ambapo watasema: “Karibu, ee nafsi nzuri iliokuwa kwenye mwili mzuri. Ingia ukiwa ni mwenye kusifiwa na pata bishara njema ya rehema, mimea yenye harufu nzuri na Mola si Mwenye kukasirika.” Hakutoacha kuendelea kusemwa hivo mpaka ifike kwenye mbingu ambayo Allaah (´Azza wa Jall) Yuko juu yake. Na kama mtu alikuwa muovu watasema: “Toka, ee nafsi ovu iliokuwa kwenye mwili mbaya. Toka ukiwa ni mwenye kusemwa vibaya na pata bishara ya maji yenye kuunguza, viza vya barafu na mfano wa hayo.” Kutaendelea kusemwa hivo mpaka pale inapotoka. Halafu ipandishwe juu mbinguni. Itaombewa idhini ya kuingia ambapo kutasemwa: “Ni nani huyu?” Kutasemwa kwamba ni fulani ambapo watasema: “Hukaribishwi, ee nafsi ovu iliokuwa kwenye mwili mbaya. Rudi hali ya kusemwa vibaya. Hakika hutofunguliwa milango ya mbinguni.” Kisha itarudishwa kutoka mbinguni mpaka ifike ndani ya kaburi.”[5][6]

Hadityh hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim licha ya kwamba hawakuipokea.

25 – Tambua ya kwamba imepokelewa kuwa Allaah yuko juu ya ´Arshi, jambo ambalo limekwishatanguliwa kutajwa, na imepokelewa pia ya kwamba Yeye (´Azza wa Jall) yuko juu ya mbingu. Mara nyingi (فِي) inakuwa kwa maana ya (على). Kama mfano wa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ

“Basi tembeeni katika (فِي) ardhi… ”[7]

Bi maana juu ya ardhi. Mfano mwingine ni:

وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ

“Nitakusulubuni katika (فِي) mashina ya mitende.”[8]

Bi maana juu ya vigogo vya mitende.  Vivyo hivyo kuhusiana na maneno Yake Allaah (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?”[9]

Bi maana Ambaye yuko juu ya mbingu. Kila kilichoko juu (علا) huitwa (سمَاء). Katika hali hiyo kinachokusudiwa kwa (السَّمَاء) ni ´Arshi ambayo ndio iko juu ya mbingu zote.

Kitendo cha Allaah (´Azza wa Jall) kuwa juu ya mbingu ni jambo limepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia ya matamshi.

[1] 67:16-17

[2] 51:22

[3] 3:55

[4] 4:158

[5] Ibn Maajah (4262) na Ahmad (2/364). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3456)

[6] Jaamiy´-ul-Bayaan (10/182-186).

[7] 9:2

[8] 20:71

[9] 67:16-17

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 50-53
  • Imechapishwa: 29/05/2024