06. Dini inamruhusu mwanamke kuonyesha uso na mikono

Maelezo haya pia yanatakiwa kuangaliwa vyema. Hata kama uso na mikono huonekana kikawaida, huonekana kwa makusudi. Ninachopata mimi kufahamu kutoka katika Aayah ni kile chenye kuonekana pasi na mtu mwenyewe kutaka. Ni vipi basi itafanywa kuwa ni dalili yenye kuenea juu ya yale yanayoonekana kwa makusudi?

Kisha baada ya hapo nikatafakari na kuona kuwa msimamo wa wanazuoni hawa ndio wa sawa na kwamba maoni yao yanatokana na umakini wa kutafakari kwao. Salaf wameafikiana juu ya kwamba maneno Yake (Ta´ala):

إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا

“… isipokuwa yale yanayodhihirika… “

yanakusudia kile kitendo kinachofanywa na yule mwanamke. Makinzano yaliyopo ni yale anayoonyesha kwa makusudi. Ibn Mas´uud anasema kuwa Aayah inakusudia nguo zake, bi maana jilbaab yake. Ibn ´Abbaas na Maswahabah wengine na wanafunzi wa Maswahabah wamesema kuwa inalenga uso na mikono yake. Kwa hiyo katika hali hiyo maana ya Aayah itakuwa isipokuwa yale ambayo Allaah amemruhusu na kumwamrisha kuyaonyesha. Je, huoni kuwa mwanamke anayepandisha jilbaab yake mpaka kukaonekana kitu katika ile nguo yake ilioko chini na mapambo yake (kama wanavofanya hivo baadhi ya wanawake wa kisaudi) anakuwa ameenda kinyume na Aayah kwa maafikiano ya wanazuoni? Kitendo chake hichi na kile cha mwanzo vyote vimefanywa kwa kutaka kwake mwenyewe. Aayah haiwezi kuwa na maana hiyo. Kwa hivyo Aayah haimlengi mwanamke asiyefanya kwa makusudi, kwa sababu hachukuliwi hatua kwa mambo anayofanya kwa kutokutaka kwake, isipokuwa yale yanayoonekana pasi na idhini kutoka kwa Allaah. Inapothibiti kuwa dini inamruhusu mwanamke kuonyesha kitu katika mapambo yake, ni mamoja ni uso, mikono au kitu kingine, basi hukumu haitakiwi kupingwa na yale makusudio tuliyoyataja. Kwa sababu dini imemruhusu kuyaonyesha kama inavyomruhusu yeye kuonyesha jilbaab. Namna hivo ndio ilikuwa mtazamo wa Maswahabah ambao wamesema kuwa kilichobaguliwa ni uso na mikono. Wanawake wengi katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada yake walikuwa wakifanya hivo, kama utakavyoona katika maandiko yanayokuja huko mbele.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 03/09/2023