Hivi hapa vitabu vyake vinatolea ushahidi tuliyoyasema. Vitabu vyake na barua zake hizi hapa ambapo ndani yake ameandika hoja alizonazo, dalili, elimu iliobobea na kufichua upotevu na utata. Ameandika yote haya. Haya kwa mfano yanapatikana katika “Kitaab-ut-Tawhiyd” na vitabu vyake vingine vinavyosapotiwa na Aayah za Qur-aan, Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya wanazuoni. Mfano wa kitabu kingine ni “Kashf-ush-Shubuhaat”. Humo mna hoja tata ambazo ulikumba ulinganizi wake na ukaenezwa na wapinzani. Amejibu hoja tata hizo na akazifichua na kuzipondaponda kwenye kijitabu hiki kidogo. Shaykh amewaraddi waliokuwa wakipingana naye kwa radd zenye kukinaisha na akabainisha upotevu wao kwa kuandika barua nyingi. Barua hizo mtazipata kwenye vitabu alivyoandika Shaykh kama “ad-Durar as-Saniyyah” na vinginevyo. Haya mtayapata yameandikwa na kuhifadhiwa na himdi zote ni za Allaah. Hali siku zote huwa hivi haki hubaki. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ

“Lakini vile vinavyowafaa watu hubakia ardhini.”

Vitabu vyake, vitabu vya wanafunzi wake na vitabu vya wafuasi wake vimebaki. Vitabu hivyo vimehifadhiwa na ni vyenye kuaminiwa na himdi zote ni za Allaah. Upande mwingine hoja tata za watatizi zimedidimia. Isitoshe vitabu vyao vimepotea na havina athari wala nafasi yoyote. Hata vile vilivyobaki katika hivyo havijulikani. Hakuna mwenye kuvikubali isipokuwa watu wa batili tu. Ama kuhusu haki iko wazi na himdi zote ni za Allaah.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 26-29
  • Imechapishwa: 07/02/2026