Haisihi twahara wala ´ibadaah nyingine katika ´ibaadah isipokuwa kwa kuitilia manuizi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika si vyenginevyo matendo yote yanategemea nia na kila mtu atapata kile alichokinuia.”[1]
Kisha aseme:
بسم الله
“Kwa jina la Allaah.”
Kisha aoshe viganja vyake mara tatu. Kisha asukutue na avute maji puani mara tatu, akiviunganisha kwa kutia maji kwa kiganja kimoja, au mara tatu. Kisha aoshe uso wake mara tatu, kuanzia sehemu zinapoota nywele za kichwa mpaka sehemu inayoteremka kwenye taya mbili na kidevu, na mpaka kwenye mashina ya masikio. Na apitishe vidole kwenye ndevu zake ikiwa ni nyingi. Ikiwa ngozi inaonekana kupitia ndevu, basi ni lazima azioshe. Kisha aoshe mikono yake mpaka kwenye viwiko mara tatu, na avijumuishe katika kuosha. Kisha apake kichwa chake pamoja na masikio; aanze kwa mikono yake kutoka sehemu ya mbele ya kichwa, kisha aipeleke mpaka nyuma ya shingo, kisha airudishe mpaka sehemu ya mbele ya kichwa. Kisha aoshe miguu yake mpaka kwenye vifundo vya miguu mara tatu, na avijumuishe katika kuosha, na apitishe vidole kati ya vidole vya miguu. Kisha anyanyue macho yake kuelekea mbinguni na aseme:
أشهدُ أن لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ و أشهدُ أنَّ محمَّدًا عبدُهُ ورسولُهُ
“Ninashuhudia ya kwamba hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”[2]
Kilicho cha wajibu katika hayo yaliyotajwa hapo juu ni: nia, kuosha kila kiungo mara mojamoja isipokuwa viganja, kupaka kichwa chote, kufuata mpangilio wa twahara kama tulivyoeleza na kutochelewesha kuosha kiungo mpaka kile kilichotangulia kikauke.
Katika hayo yaliyotajwa inapendeza kutaja jina la Allaah, kuosha viganja, kufanya kishindo katika kusukutua na kuvuta maji puani – isipokuwa ikiwa amefunga – kupitisha vidole kwenye ndevu na vidole, kupangusa masikio, kuanza upande wa kulia kabla ya upande wa kushoto, kuosha mara tatutatu. Inachukiza kuzidisha zaidi ya mara tatu na kufanya israfu katika maji.
Inapendeza kutumia Siwaak wakati harufu ya mdomo inapobadilika, wakati wa kuamka kutoka usingizini na wakati wa swalah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Lau nisingeogopa kuwatia uzito ummah wangu, basi ningewaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”[3]
Pia inapendeza kutumia Siwaak katika nyakati nyingine zote, isipokuwa kwa mwenye kufunga baada ya kupinduka kwa jua.
[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1906).
[2] Muslim (234) na at-Tirmidhiy (55).
[3] al-Bukhaariy (887) na Muslim (252).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 15-16
- Imechapishwa: 03/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 15-16
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/05-namna-ya-kutawadha/