Ni jambo linalopendeza kwa anayetaka kuingia chooni kusema:
بسم الله اللهم إني أَعُوذ بك من الخُبُثِ والخَبَائِث
“Kwa jina la Allaah. Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokamana na mashaytwaan ya kiume na ya kike.”[1]
na:
من الرِّجْسِ النِّجْسِ؛ الشَّيطانِ الرَّجيمِ
”… na kutokana na uchafu, najisi, shaytwaan aliyelaaniwa.”[2]
Wakati anapotoka aseme:
غُفْرانَكَ
“Nakuomba msamaha!”[3]
na:
الحمدُ للَّهِ الَّذي أذهبَ عنِّي الأذَى وعافاني
”Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ameniondolea madhara na akanipa afya.”[4]
Atangulize mguu wake wa kushoto wakati wa kuingia, na mguu wa kulia wakati wa kutoka. Asiingie humo akiwa na kitu chenye utajo wa Allaah (Ta´ala), isipokuwa kwa haja.
Anapokaa wakati wa kufanya haja, ajiegemeze kwenye mguu wake wa kushoto. Anapofanya haja sehemu ya wazi, aende mbali zaidi na ajisitiri na atafute sehemu laini kwa ajili ya kukojoa. Wala asikojoe kwenye tundu wala ufa, wala njia, wala kivuli chenye manufaa, wala chini ya mti wenye matunda. Wala asielekee jua wala mwezi, wala Qiblah, wala asilenge mgongo wake kuelekea Qiblah, kwa sababu ya maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msikielekee Qiblah kwa haja kubwa wala haja ndogo, wala msilenge migongo yenu kukielekea.”[5]
Hata hivyo inajuzu kufanya hivyo ndani ya majengo.
Mkojo unapokatika, afute kutoka kwenye mzizi wa uume wake kuelekea ncha yake, kisha aukamue mara tatu. Wala asiguse uume wake kwa mkono wake wa kulia, wala asijifute kwa mkono huo. Kisha ajisafishe kwa mawe kwa idadi isiyokuwa shufwa, kisha ajisafishe kwa maji. Akitosheka na kujisafisha kwa mawe, inamtosheleza ikiwa najisi haikuvuka sehemu ya kawaida. Haitoshelezi chini ya mipangusio mitatu yenye kuondoa najisi. Pia inajuzu kujisafisha kwa kila kitu kilicho twahara, isipokuwa mavi, mifupa na kitu chenye heshima.
[1] al-Bukhaariy (142) na Muslim (375).
[2] Nzuri na ngeni kwa mujibu wa Ibn Hajar katika ”Nataa-ij-ul-Afkaar” (1/198).
[3] Ahmad (25220), Abu Daawuud (30), at-Tirmidhiy (7) na Ibn Maajah (300). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (247).
[4] Ibn Maajah (301). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (57).
[5] al-Bukhaariy (144), Muslim (264), Ahmad (21), Abu Daawuud (9), at-Tirmidhiy (8), an-Nasaa’iy (21) na Ibn Maajah (318).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 14-15
- Imechapishwa: 03/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 14-15
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/04-adabu-za-kukidhi-haja/