Haijuzu kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, pasi na kujali vinatumiwa katika twahara wala katika jambo jingine. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msinywe katika vyombo vya dhahabu na fedha, wala msile katika sahani zake. Kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyenu Aakhirah.”[1]
Hukumu ya chombo kilichotiwa kiraka ni kama hukumu ya hivyo viwili. Isipokuwa ikiwa kiraka hicho ni kidogo cha fedha.
Inajuzu kutumia vyombo vingine vyote vilivyo twahara na kuvihifadhi. Inajuzu kutumia vyombo vya watu wa Kitabu na nguo zao, muda wa kuwa haijulikani kuwa ni najisi.
Sufu ya mnyama aliyekufa na nywele zake ni twahara. Kila ngozi ya mnyama aliyekufa ni najisi, ni mamoja iwe imetiwa dawa ya kusafisha ngozi au haijatiwa dawa. Kadhalika mifupa yake ni najisi. Kila mnyama aliyekufa ni najisi, isipokuwa mwanadamu na mnyama wa majini ambaye haishi isipokuwa majini tu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu bahari:
“Maji yake ni yenye kutwaharisha na mnyama wake aliyekufa ni halali.”[2]
Hukumu hiyohiyo inatumika juu ya wanyama ambao hawana damu inayotiririka, muda wa kuwa havikutokana na najisi.
[1] al-Bukhaariy (5110) na Muslim (2067).
[2] Abu Daawuud (83), at-Tirmidhiy (69), an-Nasaa’iy (59), Ibn Maajah (386), Ibn Abiy Shaybah (1/131), Ibn Khuzaymah (111), Maalik (43), ash-Shaafi´iy katika ”al-Musnad” (1/7) na Ahmad (14594).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 14
- Imechapishwa: 03/10/2026
Haijuzu kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, pasi na kujali vinatumiwa katika twahara wala katika jambo jingine. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msinywe katika vyombo vya dhahabu na fedha, wala msile katika sahani zake. Kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyenu Aakhirah.”[1]
Hukumu ya chombo kilichotiwa kiraka ni kama hukumu ya hivyo viwili. Isipokuwa ikiwa kiraka hicho ni kidogo cha fedha.
Inajuzu kutumia vyombo vingine vyote vilivyo twahara na kuvihifadhi. Inajuzu kutumia vyombo vya watu wa Kitabu na nguo zao, muda wa kuwa haijulikani kuwa ni najisi.
Sufu ya mnyama aliyekufa na nywele zake ni twahara. Kila ngozi ya mnyama aliyekufa ni najisi, ni mamoja iwe imetiwa dawa ya kusafisha ngozi au haijatiwa dawa. Kadhalika mifupa yake ni najisi. Kila mnyama aliyekufa ni najisi, isipokuwa mwanadamu na mnyama wa majini ambaye haishi isipokuwa majini tu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu bahari:
“Maji yake ni yenye kutwaharisha na mnyama wake aliyekufa ni halali.”[2]
Hukumu hiyohiyo inatumika juu ya wanyama ambao hawana damu inayotiririka, muda wa kuwa havikutokana na najisi.
[1] al-Bukhaariy (5110) na Muslim (2067).
[2] Abu Daawuud (83), at-Tirmidhiy (69), an-Nasaa’iy (59), Ibn Maajah (386), Ibn Abiy Shaybah (1/131), Ibn Khuzaymah (111), Maalik (43), ash-Shaafi´iy katika ”al-Musnad” (1/7) na Ahmad (14594).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 14
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/03-vyombo-vya-jikoni/