Nilisema katika maelezo yangu ya ”al-Jaamiy´ at-Tirmidhiy”:
”Lililo sahihi ni alilolifanya at-Tirmidhiy katika kuisahihisha Hadiyth hii. Ni Hadiyth tofauti na Hadiyth ya kupaka juu ya soksi za ngozi. Watu wamepokea kutoka kwa al-Mughiyrah Hadiyth nyingi kuhusu kupangusa katika wudhuu; miongoni mwao wapo waliopokea kupaka juu ya soksi za ngozi, wapo waliopokea kupaka juu ya kilemba na wapo waliopokea kupaka juu ya soksi za kawaida. Hakuna hata moja kati ya hizi inayopingana na nyingine, kwa sababu ni Hadiyth nyingi na riwaya za matukio tofauti. al-Mughiyrah alimsindikiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) takribani miaka mitano. Ni jambo linalokubalika kiakili kwamba ashuhudie kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) matukio mengi tofauti katika wudhuu´ wake na akayasimulia. Hivyo baadhi ya wapokezi wakasikia kutoka kwake jambo fulani na wengine wakasikia jambo jingine. Hili ni wazi na la kimsingi.”[1]
Ninaongeza juu ya hilo ya kwamba wanazuoni wamezikusanya pamoja Hadiyth zilizothibiti kuhusu sifa ya swalah ya kupatwa kwa jua au mwezi kwa njia mbalimbali, kwa kusema kwamba hii ni utofauti ya matukio, si utofauti wa mapokezi. Hali wakiwa wanajua kwamba kupatwa kwa jua au mwezi hutokea mara chache. Kwa hiyo ni bora zaidi kukusanya hivyo katika sifa ya wudhuu´ ambao hurudiwa kila siku mara nyingi. jambo hili liko wazi.
[1] Sharh Jaami´ at-Tirmidhiy (1/168).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 10
- Imechapishwa: 01/04/2026
Nilisema katika maelezo yangu ya ”al-Jaamiy´ at-Tirmidhiy”:
”Lililo sahihi ni alilolifanya at-Tirmidhiy katika kuisahihisha Hadiyth hii. Ni Hadiyth tofauti na Hadiyth ya kupaka juu ya soksi za ngozi. Watu wamepokea kutoka kwa al-Mughiyrah Hadiyth nyingi kuhusu kupangusa katika wudhuu; miongoni mwao wapo waliopokea kupaka juu ya soksi za ngozi, wapo waliopokea kupaka juu ya kilemba na wapo waliopokea kupaka juu ya soksi za kawaida. Hakuna hata moja kati ya hizi inayopingana na nyingine, kwa sababu ni Hadiyth nyingi na riwaya za matukio tofauti. al-Mughiyrah alimsindikiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) takribani miaka mitano. Ni jambo linalokubalika kiakili kwamba ashuhudie kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) matukio mengi tofauti katika wudhuu´ wake na akayasimulia. Hivyo baadhi ya wapokezi wakasikia kutoka kwake jambo fulani na wengine wakasikia jambo jingine. Hili ni wazi na la kimsingi.”[1]
Ninaongeza juu ya hilo ya kwamba wanazuoni wamezikusanya pamoja Hadiyth zilizothibiti kuhusu sifa ya swalah ya kupatwa kwa jua au mwezi kwa njia mbalimbali, kwa kusema kwamba hii ni utofauti ya matukio, si utofauti wa mapokezi. Hali wakiwa wanajua kwamba kupatwa kwa jua au mwezi hutokea mara chache. Kwa hiyo ni bora zaidi kukusanya hivyo katika sifa ya wudhuu´ ambao hurudiwa kila siku mara nyingi. jambo hili liko wazi.
[1] Sharh Jaami´ at-Tirmidhiy (1/168).
Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 10
Imechapishwa: 01/04/2026
https://firqatunnajia.com/05-matukio-mawili-tofauti/