05. Kwenda Misri kwa ajili tu ya Hadiyth moja

31 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mughiyrah, ambaye amesema:

”Kulisemwa kuambiwa Sa´iyd bin Jubayr: ”Unamjua mtu ambaye ni mjuzi zaidi kuliko wewe?” Akasema: ”Ndio. ´Ikrimah.” Wakati Sa´iyd bin Jubayr alipouliwa, Ibraahiym akasema: ”Hajaacha nyuma yake mtu kama yeye.” Wakati ash-Sha´biy alipopata khabari kuwa Ibraahiym amefariki, akasema: ”Mtu huyo amekufa?” Kukasemwa: ”Ndio.” Ndipo akasema: ”Ningelikuwa natoa hukumu ya kifo juu ya elimu, ningesema kuwa hajamwacha yeyote baada yake mfano wake.” Jambo la kushangaza ni kuwa anamfadhilisha Ibn Jubayr juu ya nafsi yake. Nitakwelezeni juu ya hilo; amekulia kwenye nyumba ya watu walio na uelewa na akachukua uelewa wao. Kisha akaketi na sisi, akachukua Hadiyth zetu bora na akaziongeza juu ya uelewa wa watu wa nyumbani kwake. Ni nani atakuwa kama yeye?”

32 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia: Ayyuub at-Twaa-iy ametuhadithia: Nimemsikia ash-Sha´biy akisema:

”Sijamuona mtu yeyote ulimwengu anayetafuta elimu kama Masruuq.”

33 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia, kutoka kwa Jariyr bin Hayyaan, ambaye amesema:

”Bwana mmoja[1] alisafiri kwenda Misri kwa ajili tu ya Hadiyth hii:

”Yule anayemsitiri ndugu yake duniani, Allaah atamsitiri Aakhirah.”

Kipando chake hakikuwahi kufika kabla ya kurejea nyumbani kwake.”

34 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Jurayj, aliyesema:

”Naafiy´ alinisomea.”

35 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr, kutoka kwa Warraad, mwandishi wa al-Mughiyrah, ambaye amesema:

”al-Mughiyrah alinisomea. Na mimi huku nikiandika kwa mkono wangu.”

36 – Abu Khaythamah ametuhadithia: ´Abdullaah bin Numayr ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, ambaye amesema:

”Ibraahiym alitaja faradhi au Hadiyth akasema: ”Ihifadhi hii. Pengine ukaulizwa nayo siku katika siku.”

37 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym, ambaye amesema:

”Walikuwa wakichukia mtu kuonyesha kile alichonacho.”

38 – Abu Khaythamah ametuhadithia: ´Aththaam bin ´Aliy al-´Aamiriy ametuhadithia: Nimemsikia al-A´mash akisema:

”Sijwahi kumsikia hata siku moja Ibraahiym akisema kitu kwa maoni yake.”

[1] Bi maana ´Uqbah bin ´Aamir. Alisafiri kwenda kwa Maslamah bin Makhlad, ambaye alikuwa mwana wa mfalme huko Misri, kama ilivyo katika “al-Musnad” (4/104).

  • Mhusika: Imaam Abu Khaythamah Zuhayr bin Harb an-Nasaa’iy (afk. 234)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-´Ilm, uk. 18-20
  • Imechapishwa: 17/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy