Imepokelewa mahimizo ya kusoma koo za watu kwa ajili ya kuunga udugu. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jifunzeni nasaba zenu kwa kiasi kitachokuwezesheni kuunga kizazi chenu.”[1]

Ameipokea Ahmad na at-Tirmidhiy.

Humayd bin Zanjuuyah ameipokea kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Jifunzeni nasaba zenu kwa kiasi kitachokuwezesheni kuunga kizazi chenu, na si zaidi ya hivyo.” Jifunzeni kiarabu kwa kiasi kitachokuwezesheni kukijua Kitabu cha Allaah, na si zaidi ya hivyo. Jifunzeni nyota kwa kiasi kitachokuwezesheni kukuongozeni katika viza vya bahari na nchikavu, na si zaidi ya hivyo.”[2]

Katika cheni ya wapokezi wake yuko Ibn Lahiy´ah. Ameipokea pia kupitia kwa Nu´aym bin Abiy Hind ambaye ameeleza kwamba ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Jifunzeni nyota kiasi ambacho kitakuongozeni katika nchikavu na baharini mwenu, kisha jizuieni. Jifunzeni nasaba zenu kwa kiasi kitachokuwezesheni kuunga kizazi chenu, na si zaidi ya hivyo. Jifunzeni kile kiasi kitachokufanyeni kujua yale ambayo ni halali kwa wanawake na yale ambayo ni haramu kwenu, na si zaidi ya hivyo.”

Mis´ar amesimulia kupitia kwa Muhammad bin ´Ubayd ambaye amesema kuwa ´Umar amesema:

“Jifunzeni nyota kwa kiasi kitachokufanyeni kujua Qiblah na njia.”

[1]Ahmad (2/374) na at-Tirmidhiy (1979). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (1979).

[2]al-Bayhaqiy katika “Shu’b-ul-Iymaan” (1594).

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 13/09/2021