Imaam Ibn-ul-Qayyim amezungumzia kwa maneno yenye nguvu na mazuri kuhusu Hadiyth hii na suala hili, japokuwa siafikianii naye katika kuidhoofisha Hadiyth hii ya al-Mughiyrah. Amesema:
”an-Nasaa’iy amesema:
”Hatumjui yeyote aliyemfuata Huzayl katika riwaya hii. Lililo sahihi kutoka kwa al-Mughiyrah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipangusa juu ya soksi za ngozi.”
al-Bayhaqiy amesema:
”Abu Muhammad – yaani Yahyaa bin Mansuur – amesema: ”Nilimwona Muslim bin al-Hajjaaj akiidhofisha Hadiyth hii.” Amesema tena: ”Abu Qays al-Awdiy na Huzayl bin Shurahbiyl hawawezi kubeba riwaya hii, pamoja na kupingana kwao na kundi la wapokezi waliopokea Hadiyth hii kutoka kwa al-Mughiyrah, waliotaja kupangusa juu ya soksi zenye ngozi.” Amesema tena: ”Haiachwi dhahiri ya Qur-aan kwa mfano wa Abu Qays na Huzayl.” Akasema: ”Nikamtajia Abul-‘Abbaas ad-Dughuliy simulizi hii kutoka kwa Muslim, naye akasema: ”Nilimsikia ‘Aliy bin Makhlad bin Sufyaan akisema: Nilimsikia Abu Qudaamah as-Sarkhasiy akisema: ‘Abdur-Rahmaan bin Mahdiy amesema: Nilimwambia Sufyaan ath-Thawriy: ”Kama mtu angenisimulia Hadiyth ya Abu Qays kutoka kwa Huzayl nisingeipokea.” Ndipo Sufyaan akasema: ”Hadiyth ni dhaifu, nyonge au neno kama hilo.”
‘Abdullaah bin Ahmad amesema: ”Nilimuhadithia baba yangu Hadiyth hii, baba yangu akasema: ”Hadiyth hii haipokelewi isipokuwa kupitia Abu Qays.” Baba yangu akasema tena: ”‘Abdur-Rahmaan bin Mahdiy alikataa kuisimulia akisema kuwa ni dhaifu na yenye kupingana.”
‘Aliy bin al-Madiyniy amesema:
”Hadiyth ya al-Mughiyrah bin Shu‘bah kuhusu kupaka imepokelewa kutoka kwake na watu wa Madiynah, watu wa Kuufah na watu wa Baswrah. Huzayl bin Shurahbiyl pia ameipokea kutoka kwa al-Mughiyrah isipokuwa akasema: ”Alipaka juu ya soksi za ngozi na akaenda kinyume na watu.”
al-Fadhwl bin ‘Utbaan amesema:
”Nilimuuliza Yahyaa bin Ma‘iyn kuhusu Hadiyth hii, akasema: ”Watu wote wanaipokea kuwa ni kupaka juu ya soksi za ngozi isipokuwa Abu Qays.”
Ibn-ul-Mundhir amesema:
”Kupaka juu ya soksi kumepokelewa kutoka kwa Maswahabah tisa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): ‘Aliy, ‘Ammaar, Abu Mas‘uud al-Answaariy, Anas, Ibn ‘Umar, al-Baraa’, Bilaal, ‘Abdullaah bin Abi Awfaa na Sahl bin Sa‘d.”
Abu Daawuud akamwongoza Abu Umaamah, ‘Amr bin Hurayth, ‘Umar na Ibn ‘Abbaas.”
Basi hawa ni Maswahabah kumi na watatu. Msingi wa uhalali unatokana na hawa (Radhiya Allaahu ‘anhum), si juu ya Hadiyth ya Abu Qays.
Pamoja na kwamba wanaopinga kupaka wanajikinzana. Kwa sababu lau Hadiyth hii ingekuwa upande wao wangesema kuwa hiyo ni ziada na ziada kutoka kwa mtu mwenye kuaminika ni yenye kukubalika na wangefumbia macho yale yote waliyoyataja hapa kuhusu kupwekeka kwa Abu Qays katika kuisimulia. Lakini Hadiyth inapokuwa dhidi yao wanaidhoofisha kwa sababu ya upweke wa mpokezi na wala hawasemi ziada ya mwenye kuaminika ni yenye kukubalika, kama inavyoonekana katika mwenendo wao. Uadilifu ni kumpimia mpinzani wako kwa kipimo kilekile unachojipimia wewe mwenyewe, kwani katika mambo yote kuna kutimiza au kupunguza. Sisi hatukubali njia hii. Wala hatujengei hoja kwa Hadiyth ya Abu Qays. Imaam Ahmad ameeleza kwa uwazi juu ya kufaa kupangusa juu ya soksi za ngozi na akaieleza sababu ya Hadiyth ya Abu Qays. Hili ni miongoni mwa inswafu na uadilifu wake (Rahimahu Allaah). Msingi wake ni hawa Maswahabah na kipimo cha wazi, kwani haionekani tofauti yenye athari kati ya soksi na soksi za ngozi inayofaa kuhamishiwa hukumu juu yake.”[1]
Hidi ndivo alivyosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah). Sisi tunampinga katika kuitia kasoro Hadiyth ya Abu Qays kutoka kwa Huzayl. Kwa sababu riwaya za Maswahabah wa al-Mughiyrah kutoka kwake katika Hadiyth hii kwamba kulikuwa na kupaka juu ya soksi za ngozi hazikanushi usahihi wa riwaya ya Huzayl bin Shurahbiyl kutoka kwake kuhusu kupaka juu ya soksi za kawaida. Hili ni tukio na lile ni tukio jingine.
[1] Tahdhiyb-us-Sunan (1/121-122).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 7-11
- Imechapishwa: 31/03/2026

Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 7-11
Imechapishwa: 31/03/2026
https://firqatunnajia.com/04-sababu-ya-ibn-ul-qayyim-kujuzisha-kupangusa-juu-ya-soksi-za-kitambaa/