Shaykh (Rahimahu Allaah) akaamrisha jihaad. Kukaandaliwa jeshi litalopambana na mwenye kuizuia dini ya Allaah na kukataa kukubali haki na kutaka kuendelea katika shirki na batili. Bendera ya jihaad katika njia ya Allaah ikasimama. Kuamrisha mema na kukataza maovu kukapamba moto. Kuhukumu kwa Shari´ah kukapamba moto badala ya hukumu na desturi za kikabila. Hukumu ya Shari´ah iliyosafi kabisa ikasimama katika nchi hii. Nuru ya ulingano ikaenea katika miji jirani ya Dar´iyyah na jihaad katika njia ya Allaah ikashika moto ambapo wakawa wanapambana na wale wenye kuzuia na njia ya Allaah na wakati huohuo anakataa kukubali haki. Kuhusiana na yule mwenye kumuamini Allaah, akakubali ulinganizi na hakuleta vipingamizi, basi akabaki katika utukufu wake, hadhi yake na Allaah akazidi kumnyanyua zaidi. Kuhusiana na wale wenye kuzuia dini ya Allaah, basi Allaah aliwanusuru watu wa haki dhidi ya wapinzani.
Ulinganizi wa Shaykh ukaenea na hukumu ya familia ya Muhammad bin Su´uud ikaenea katika miji ilio pambizoni. Baada ya yeye kuwa ni kiongozi wa mji mmoja akawa ni kiongozi wa miji yote ya Najd. Sivyo tu bali hukumu ya familia ya Su´uud, hukumu ya Shari´ah na Tawhiyd ikaenea Hijaaz, Yemen, miji ya Shaam na ikatapakaa sehemu kubwa ya kisiwa cha waarabu. Ulinganizi ukaenea pande za kizazi cha Su´uud na ufalme wake ukaenea sehemu kubwa ya kisiwa cha waarabu. Hivyo Tawhiyd ikaeneza na ´Aqiydah ikadhihiri. Watu wakanufaika na nuru na I´tiqaad mbovu walizokuwa nazo zikaondoka. Allaah akawanusuru watu na mashaytwaan ambao wanawazuia na kuwalia mali zao kwa kutumia jina la elimu na jina la uongozi. Watu hawa walikuwa wakiwaongoza watu kwa ukhurafi na wakiwalia mali zao kwa dhuluma, madhambi na uadui. Hata hivyo yote haya yakaondoka na himdi zote ni za Allaah. Yote haya aliyokuwa akifanya Shaykh hakuna alichokuwa anataka isipokuwa thawabu kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hakuwa anataka watu wamsifu, hakutaka kuwa na uongozi juu ya watu na wala hakuwa anataka kukusanya pesa. Bali Shaykh alikuwa akitoa pesa zake mpaka akifikia kuchua deni ili aweze kutoa katika njia ya Allaah, akiwapa wanafunzi na wasafiri waliokuja kusoma wasiokuwa na makazi. Watu kama hawa Shaykh alikuwa akiwahudumia kiasi na uwezo wake. Amekufa (Rahimahu Allaah) ilihali ni fakiri hana pesa. Lakini hata hivyo amekufa ilihali yuko na ujira na thawabu za kutosha kwa kueneza elimu na ulinganizi mpaka dini ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ikaweza kudhihiri. Amesema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ
“Yeye ndiye Aliyemtuma mtume Wake kwa mwongozo na dini ya haki ili aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.”
Hii ndio historia kuhusu ulinganizi wa Shaykh kwa ufupi.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 22-26
- Imechapishwa: 07/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 22-26
Imechapishwa: 07/02/2026
https://firqatunnajia.com/04-namna-ulivyoenea-ulinganizi-wa-shaykh-katika-kisiwa-cha-kiarabu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket