Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Suala la pili: Kuifanyia kazi

MAELEZO

Kuifanyia kazi – Matendo yanayopelekea utambuzi huu. Kama vile kumwamini Allaah, kumtii, kutekeleza maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake katika aina za ´ibaadah maalum na aina elekezi ya ´ibaadah. ´Ibaadah ambazo ni maalum ni mfano wa swalah, swawm na hajj. ´Ibaadah ambazo ni elekezi ni mfano wa kuamrisha mema, kukataza maovu, kupambana nihaad katika njia ya Allaah na mfano wa hayo.

Uhakika wa mambo ni kwamba matendo ndio matunda ya ujuzi. Yule mwenye kutenda pasi na ujuzi, basi amejishabihisha na wakristo, wakati yule mwenye kujua na asitende, basi amejishabihisha na mayahudi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 21
  • Imechapishwa: 16/05/2020