4 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mbali na wale Malaika wanaoandika matendo ya watu Allaah anao Malaika wanaozunguka ardhini. Wanapowapata watu wanaomdhukuru Allaah (Ta´ala) wanaita: “Njooni katika utashi wenu!” Kisha wanawazunguka. Wanapotawanyika wanapanda mbinguni ambapo Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anasema: “Mmewaacha waja wangu wanafanya nini mlipowaacha?” Wanasema: “Tumewaacha wanakuhimidi, wanakutukuza na wanakutaja.” Ndipo aseme: “Kwani wamekwishaniona?” Wanasema: “Hapana.”Aseme: “Vipi lau wangeniona?” Waseme: “Lau wangekuona basi wangekuhimidi, kukutukuza na kukutaja kwa wingi kulikoni.”Aseme: “Kwani wanatafuta nini?” Waseme: “Wanatafuta Pepo.” Aseme: “Wamekwishaiona?” Waseme: “Hapana.”Aseme: “Vipi lau wangeiona?”Waseme: “Wangeiona basi wangelikuwa na bidii zaidi kulikoni.”Aseme: “Wanajilinda kutokamana na nini?” Waseme: “Wanajilinda kutokamana na Moto.”Aseme: “Kwani wamekwishauona?” Waseme: “Hapana.” Aseme: “Vipi wangeuona?” Waseme: “Wangeuona basi wangeukimbia na kujilinda nao zaidi kulikoni.”Ndipo aseme: “Mimi nakushuhudisheni kwamba nimewasamehe.” Waseme: “Wako ambao wameingia kimakosa. Wameingia humo kwa ajili ya tu haja.”Aseme: “Ni watu ambao matangamano yao si yenye kula khasara. Ni watu ambao matangamano yao si yenye kula khasara.”[1]
Tamko ni la al-Bukhaariy.
MAELEZO
Hadiyth hii inafahamisha ubora wa vikao vya dhikr na kwamba Malaika wanawafunika kwa mbawa zao.
Hadiyth pia inafahamisha fadhilah za wanaume na wanawake wenye kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).
Hadiyth pia inajulisha kuwa Allaah anawasamehe wenye kumtaja, jambo ambalo ni fadhilah kuu.
Hadiyth pia inajulisha kuwa rehema zinawaenea wenye kumtaja na wale walio pamoja nao ingawa hawatokani nao. Ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ni watu ambao matangamano yao si yenye kula khasara.”
[1] al-Bukhaariy (6408) na Muslim (4689).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 10-11
- Imechapishwa: 24/09/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 10-11
Imechapishwa: 24/09/2025
https://firqatunnajia.com/04-malaika-wanaotafuta-vikao-vinavyomtaja-allaah/