Kupinda kutoka katika ´Aqiydah sahihi ni maangamivu na khasara. ´Aqiydah sahihi ndio ngao yenye nguvu inayopelekea katika matendo yenye kunufaisha. Mtu kukaa hivihivi bila ya kuwa na ´Aqiydah sahihi anakuwa ni mateka wa fikira na mashaka mbalimbali ambayo huenda yakamfanya kuingia ndani yake. Hayo yakamzuia kutokamana na maono sahihi ya kuweza kuyapata maisha yenye furaha kiasi cha kwamba mpaka maisha yake yakawa ni yenye dhiki. Matokeo yake anakuwa ni mwenye kujaribu kutoka katika matatizo haya japokuwa kwa kujilipua, kama wafanyavo wengi ambao wamekoseshwa kuongozwa katika ´Aqiydah sahihi.
Jamii ambayo haiongozwi kwa ´Aqiydah sahihi ni jamii ya kinyama ambayo imepoteza nyenzo zote za maisha yenye furaha. Haijalishi kitu japokuwa itakuwa ni yenye kumiliki nyenzo zote za mambo ya kiuchumi yanayopelekea katika maisha yenye furaha, ambayo mara nyingi yanaipelekea katika maangamivu. Hayo yanaonekena katika jamii ya kikafiri. Nyenzo hizi za kiuchumi zinahitajia miongozo na maelekezo ili zifaidike kutoka katika sifa na manufaa yake. Hakuna miongozo mingine zaidi ya ´Aqiydah sahihi. Amesema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
“Enyi Mitume! Kuleni katika vizuri na fanyeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo ni mjuzi.”[1]
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا ۖ يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ ۖ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ ۖ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ ۖ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ ۖ وَمِنَ الْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ ۚ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ
”Hakika Tulimpa Daawuud fadhilah kutoka Kwetu [tukasema]: ”Ee milima! Rejesheni kumtukuza pamoja naye na ndege pia na tukamlainishia chuma na kwamba: ”Tengenezeni mavazi ya chuma mapana na kadiria sawasawa katika kuunganisha daraya na fanyeni mema, hakika Mimi ni Mwenye kuona myatendayo. Na kwa Sulaymaan tulimuitishia upepo; safari yake ya asubuhi ni mwezi, na safari yake ya jioni ni mwezi, na tukamtiririzia chemchemu za shaba. Na miongoni mwa majini wanaofanyia kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake. Na yeyote atakayezikengeuka amri Zetu tutamuonjesha adhabu ya Moto uliowashwa vikali mno. Wanamfanyia kazi atakayo [kujenga] ngome ndefu za fakhari na tasawiri na madeste makubwa kama mahodhi na masufuria makubwa yaliyothibiti imara. [Tukasema]: ”Fanyeni, enyi familia ya Daawuud, kwa shukurani! – na ni wachache miongoni mwa waja Wangu ni wenye kushukuru.”[2]
Nguvu ya ´Aqiydah inatakiwa iende sambamba na nguvu za kiuchumi. Ikiachana nayo na badala yake ikaenda kushika I´tiqaad ambazo ni batili, basi nguvu hizi za kiuchumi zinakuwa ni njia inayopelekea katika maangamivu. Hayo yanaonekana hii leo katika miji ya makafiri ambayo yanamiliki uchumi pasi na kumiliki ´Aqiydah sahihi.
[1] 23:51
[2] 34:10-13
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 09-11
- Imechapishwa: 22/01/2020

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 09-11
Imechapishwa: 22/01/2020
https://firqatunnajia.com/03-sura-ya-tatu-kupondoka-katika-aqiydah-na-njia-ya-kujiepusha-nalo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)