[4] Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na haikuumbwa pasi na kujali namna itakavyosomwa na namna itakavyoandikwa na popote pale itakaponakiliwa. Kitabu ni yale yaliyoandikwa, kisomo ni yale yanayosomwa. Maneno ya Allaah ni ya kale [milele] na hayakuumbwa katika hali zote. Ni maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa, hayakuzuliwa wala kutengenezwa kwa hali yoyote ile. Wala sio mwili, kiungo, jauhari wala aradhi, Bali ni sifa moja katika sifa za kidhati zinazotofautiana na viumbe vyote.
[5] Hakuacha na bado ni mwenye kuendelea kuzungumza. Maneno Yake hayawezi kutengana na dhati Yake. Wakati fulani yanasikika kutoka Kwake (´Azza wa Jall) na wakati mwingine yanasisika kutoka kwa msomaji. Yule mwenye kuyasikia moja kwa moja kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye aliyepokea uzungumzishwaji mwenyewe pasi na mkatikati wala mkalimani. Kwa mfano Allaah alimzungumzisha Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni. Kadhalika aliongea na Muusa kwenye mlima wa Sinai. Vivyo hivyo Malaika wanaozungumzishwa Naye. Vinginevyo, maneno ya Allaah ya kale yanasikika kikweli kutoka kwa msomaji na yana herufi zenye kufahamika na sauti yenye kusikika.
- Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 23-24
- Imechapishwa: 20/02/2019
[4] Qur-aan ni maneno ya Allaah yaliyoteremshwa na haikuumbwa pasi na kujali namna itakavyosomwa na namna itakavyoandikwa na popote pale itakaponakiliwa. Kitabu ni yale yaliyoandikwa, kisomo ni yale yanayosomwa. Maneno ya Allaah ni ya kale [milele] na hayakuumbwa katika hali zote. Ni maneno ya Allaah ambayo hayakuumbwa, hayakuzuliwa wala kutengenezwa kwa hali yoyote ile. Wala sio mwili, kiungo, jauhari wala aradhi, Bali ni sifa moja katika sifa za kidhati zinazotofautiana na viumbe vyote.
[5] Hakuacha na bado ni mwenye kuendelea kuzungumza. Maneno Yake hayawezi kutengana na dhati Yake. Wakati fulani yanasikika kutoka Kwake (´Azza wa Jall) na wakati mwingine yanasisika kutoka kwa msomaji. Yule mwenye kuyasikia moja kwa moja kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye aliyepokea uzungumzishwaji mwenyewe pasi na mkatikati wala mkalimani. Kwa mfano Allaah alimzungumzisha Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa kupandishwa mbinguni. Kadhalika aliongea na Muusa kwenye mlima wa Sinai. Vivyo hivyo Malaika wanaozungumzishwa Naye. Vinginevyo, maneno ya Allaah ya kale yanasikika kikweli kutoka kwa msomaji na yana herufi zenye kufahamika na sauti yenye kusikika.
Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 23-24
Imechapishwa: 20/02/2019
https://firqatunnajia.com/03-sauti-ya-allaah-ni-yenye-kusikika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)