03. Mfano wa matendo mema yanayofanywa katika kumi la kwanza la Dhul-Hijjah

Katika siku hizi kuna matendo yenye fadhilah nyingi na utiifu mwingi ikiwa ni pamoja na:

1 – Kuzidisha swalah za Sunnah, swadaqah na matendo mengine mema kama kuwafanyia wema wazazi, kuunga ukoo, tawbah ya kweli na kurejea kwa Allaah kwa unyenyekevu.

2 – Kuzidisha kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kusema ”Allaahu Akbar” na kusoma Qur-aan.

3 – Funga. Hata kama hakuna Hadiyth maalum inayohusisha funga ya siku tisa za Dhul-Hijjah, lakini kufunga ni miongoni mwa matendo bora yaliyohimizwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo inapata kufahamika kuwa kufunga siku hiyo ni jambo linalopendeza kutokana na dalili za jumla.

4 – Kufanya Hajj na ´Umrah, ambayo ni miongoni mwa matendo bora kabisa, kama itakavyokuja – Allaah akitaka.

5 – Kufanya bidii kuchinja Udhhiyah na kutolichukulia jambo hili kwa wepesi, kwa sababu ya ujira wake mkubwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
  • Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 6-7
  • Imechapishwa: 04/05/2025