03. Haisihi imani ya yeyote mpaka aamini nguzo sita za imani

Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, kufufuliwa baada ya mauti na kuamini Qadar; kheri yake na shari yake.

MAELEZO

Nayo ni: – Bi maana ndio I´tiqaad ya al-Firqah an-Naajiyah.

Imani – Imani maana yake kilugha ni kusadikisha. Allaah (Ta´ala) amesema katika Aayah ya 17 kutoka katika Suurah “Yuusuf”:

وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ

“Nawe si mwenye kutumuamini japo tukiwa ni wakweli.”[1]

Bi maana mwenye kutusadikisha.

Kuhusu maana yake Kishari´ah ni kutamka kwa ulimi, kuamini kwa moyo na matendo ya viungo.

Kumuamini Allaah, Malaika… – Hizi ndio nguzo za imani sita ambazo haisihi imani ya yeyote mpaka pale atapoziamini zote kwa njia sahihi ambayo imefahamishwa na Qur-aan na Sunnah. Nguzo zenyewe ni hizi zifuatazo:

[1] 12:17

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 06-07
  • Imechapishwa: 07/02/2018

Turn on/off menu