2 – Ama Hadiyth ya al-Mughiyrah bin Shu‘bah ameipokea Imaam. Pia ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan, Ibn Maajah, Ibn Hazm katika “al-Muhallaa” na al-Bayhaqiy katika “as-Sunan al-Kubraa”, wote hao kupitia kwa Sufyaan ath-Thawriy, kutoka kwa Abu Qays, kutoka kwa Huzayl bin Shurahbiyl, kutoka kwa al-Mughiyrah bin Shu´bah. at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
Abu Daawuud amesema baada ya upokezi wake:
”‘Abdur-Rahmaan bin Mahdiy alikuwa hasimulii Hadiyth hii, kwa sababu kinachojulikana kutoka kwa al-Mughiyrah ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipaka juu ya ngozi za soksi.”[1]
Maneno ya wanazuoni waliotaka kuitia kasoro Hadiyth hii yote yanazunguka kwenye kitendo hiki cha ‘Abdur-Rahmaan bin Mahdiy. Hadiyth hii ni Swahiyh na cheni yake ya wapokezi wote ni wenye kuaminika.
Abu Qays ‘Abdur-Rahmaan bin Tharwaan al-Awdiy alikuwa ni mtu madhubuti. Ibn Ma´iyn amemzingatia kuwa ni madhubuti na al-´Ijliy amesema:
”Madhubuti na thabiti.”
Vilevile al-Bukhaariy amesimulia Hadiyth zake katika ”as-Swahiyh” yake. Ni kweli kuwa Imaam Ahmad amesema kuwa alikuwa anaweza kukhitalifiana katika Hadiyth zake, lakini hakukusudia kujeruhi uaminifu wake, bali alikusudia kuitia kasoro Hadiyth hii. Kwa sababu alikuwa anaona kuwa amewapinga wapokezi wengine wa Hadiyth hiyo. Itakuja kubainishwa kuwa upinzani huu haudhuru NA wala haufai kuwa sababu ya kuidhoofisha Hadiyth.
Huzayl bin Shurahbiyl al-Awdiy ni Taabi‘iy wa zamani. Inasemekana alikutana na zama za kabla ya kuja Uislamu. Alikuwa ni mtu madhubuti bila ya kipingamizi. Unaweza kupata wasifu wake katika ”Twabaqaat” (6/122) ya Ibn Sa‘d, katika ”at-Taariykh al-Kabiyr” (4/2/245) ya al-Bukhaariy na katika ”al-Iswaabah” (6/303) ya Ibn Hajar.
[1] as-Sunan (159).
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 3-4
- Imechapishwa: 31/03/2026

Muhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir (afk. 1377)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 3-4
Imechapishwa: 31/03/2026
https://firqatunnajia.com/03-hadiyth-ya-al-mughiyrah-kuhusu-kupangusa-juu-ya-soksi-ni-swahiyh/