03. Hadiyth ”Siku hiyo ndio ambayo Mola wako amelingana juu ya ´Arshi… ”

Hadiyth ya pili

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

2 – Abu ´Abdillaah Muhammad bin al-Husayn al-Faramiy ametukhabarisha Misri: Muhammad bin ´Imaad ametuhadithia: ´Abdullaah bin Rafaa´ah ametuhadithia: ´Aliy bin al-Hasan ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin al-Haajj ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad as-Swaabuuniy ametuhadithia kwa kutusomea: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametuhadithia: ash-Shaafi´iy ametuhadithia: Ibraahiym bin Muhammad ametuhadithia: Muusa bin ´Ubaydah amenihadithia: Mu´aawiyah bin Ishaaq bin Twalhah amenihadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umayr ambaye amesimulia kuwa amemsikia Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) akisema:

”Jibriyl (´alayhis-Salaam) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na kioo cheupe na kilicho na doa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Nini hiki?” Akasema: ”Hii ni siku ya ijumaa… Wataipenda siku ya ijumaa kutokana na zile kheri ambazo Mola wao anawatunuku. Siku hiyo ndio ambayo Mola wako amelingana juu ya ´Arshi, akaumbwa Aadam na itasimama Saa.”[2]

Hadiyth hii ni geni. ash-Shaafi´iy ameipokea katika ”al-Musnad”. Katika cheni ya wapokezi kuna wapokezi wawili wanyonge: Muusa na Ibraahiym bin Abiy Yahyaa.

3 – Ishaaq bin Raahuuyah amesema: Nimemsikia Bishr bin ´Umar akisema: Nimewasikia wafasiri wengi wakisema:

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”

”Bi maana amenyanyuka (ارتفع).”

Abul-´Aaliyah pia amesema hivo.

4 – al-Bukhaariy amesema katika ”as-Swahiyh” yake:

”Mujaahid amesema:

”Amelingana (اسْتَوَى) maana yake ni kwamba Yuko juu (علا) ya ´Arshi.”

5 – Daaraqutwniy amepokea kutoka kwa Ishaaq al-Haadiy: Nimemsikia Abul-´Abbaas Tha´lab akisema kuhusu:

ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ

”Kisha اسْتَوَى juu ya ´Arshi.”[3]

”Bi maana yuko juu (علا) ya ´Arshi.”[4]

06 – Muhammad bin Jariyr at-Twabariy amesema kuhusu:

ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ

”Kisha اسْتَوَى juu ya ´Arshi.”

”Mwingi wa huruma anasema kuwa yuko juu (علا) na amepanda (ارتفع) juu ya ´Arshi.”[5]

[1] 20:5

[2] ash-Shaafi´iy amesema katika ”al-Musnad” (374). adh-Dhahabiy amesema:

”Ibraahiym na Muusa ni wanyonge.” (al-´Uluww, uk. 30)

[3] 7:54

[4] Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (3/387-402).

[5] Jaamiy´-ul-Bayaan (16/11).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 34-37
  • Imechapishwa: 28/05/2024