739- Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Nilikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika safari miongoni mwa safari ambapo nikawa karibu naye na huku tunasafiri. Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nijuze juu ya kitendo kitachoniingiza Peponi na kitanitenga mbali na Moto?” Akasema: “Hakika umeuliza juu ya jambo kubwa, lakini ni jepesi kwa yule aliyewepesishiwa na Allaah; mwabudu Allaah na wala usimshirikishe Yeye na chochote, simamisha swalah, toa zakaah, funga Ramadhaan na uhiji Nyumba.”[1]
Ameipokea Ahmad, at-Tirmidhiy ambaye ameihihisha, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.
[1] Swahiyh kupitia zengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/456)
- Imechapishwa: 12/05/2020
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket