22 – al-Agharr bin Yasaar al-Muzaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Enyi watu! Tubuni kwa Allaah. Kwani hakika mimi natubia Kwake mara mia kwa siku.”[1]
Ameipokea Muslim.
23 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Naapa kwa Allaah! Hakika mimi namwomba Allaah msamaha na kutubia Kwake kwa siku zaidi ya mara sabini.”[2]
Ameipoke al-Bukhaariy.
MAELEZO
Hadiyth hizi mbili kuna kusuniwa kuomba msamaha na kutubu. Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaomba msamaha katika kikao kimoja mara mia, ilihali Allaah amekwishamsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja huko mbele, tusemeje sisi?
Hakika mambo yalivyo ni kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo – ilihali Allaah amekwishamsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja huko mbele – kwa ajili ya kumwabudu Allaah, kumshukuru na ili ummah waweze kumuigiliza yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (2702).
[2] al-Bukhaariy (6307).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 28
- Imechapishwa: 05/10/2025
22 – al-Agharr bin Yasaar al-Muzaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Enyi watu! Tubuni kwa Allaah. Kwani hakika mimi natubia Kwake mara mia kwa siku.”[1]
Ameipokea Muslim.
23 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Naapa kwa Allaah! Hakika mimi namwomba Allaah msamaha na kutubia Kwake kwa siku zaidi ya mara sabini.”[2]
Ameipoke al-Bukhaariy.
MAELEZO
Hadiyth hizi mbili kuna kusuniwa kuomba msamaha na kutubu. Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaomba msamaha katika kikao kimoja mara mia, ilihali Allaah amekwishamsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja huko mbele, tusemeje sisi?
Hakika mambo yalivyo ni kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo – ilihali Allaah amekwishamsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yatayokuja huko mbele – kwa ajili ya kumwabudu Allaah, kumshukuru na ili ummah waweze kumuigiliza yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (2702).
[2] al-Bukhaariy (6307).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 28
Imechapishwa: 05/10/2025
https://firqatunnajia.com/02-mtume-akiomba-msamaha-kwa-siku-mara-mia/