Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:
na kubainisha kinyume chake ambacho ni kumshirikisha Allaah.
MAELEZO
Kinyume cha Tawhiyd ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Tawhiyd ni kumpwekesha Allaah katika ´ibaadah na shirki ni kufanya kitu miongoni mwa aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jall). Mfano wa hayo ni kuchinja, kuweka nadhiri, kuomba du´aa, uokozi na aina nyinginezo za ´ibaadah. Hii ndio shirki. Makusudio ya shirki ni katika ´ibaadah. Ama kuhusu shirki katika Rubuubiyyah ni kitu kisichokuwepo mara nyingi. Watu wote ni wenye kuikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Hili hawana namna ya kulikwepa. Mwenye kuipinga anajidhihirisha hivyo pamoja na kuwa wakati huohuo anaikubali ndani ya moyo wake. Kwa sababu kuikubali ni kitu kisichokuwa na budi. Kila mtu anajua kuwa viumbe hivi na ulimwengu huu ni lazima uwe na Muumbaji na ulimwengu huu unaoenda ni lazima uwe na mwendeshaji. Ulimwengu huu hauko bure tu hivihivi kwa dhati yake:
أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ
“Au wameumbwa pasipo na kitu chochote au wao [wenyewe] ndio waumbaji? Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini. (53:35-36)
Kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni kitu cha kilazima na tena cha kimaumbile. Hata hivyo ni kitu kisichotosheleza. Kule washirikina kuikubali hakukuwatosheleza kitu kama ilivyotajwa katika Qur-aan. Qur-aan imetaja jambo hili waziwazi:
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ
“Na ukiwauliza: “Ni nani kawaumba?”
Wanajibu nini?
Wanajibu kwa kusema:
اللَّـهُ
“Allaah.” (43:87)
Bi maana Allaah Ndiye ambaye ametuumba. Hii ndio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Kinachotakikana ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Hapa ndipo kulitokea tofauti na magomvi baina ya Mitume na nyumati zao, wenye kulingania katika dini ya Allaah na watu. Mizozo, mapambano, kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah na mengineyo yanapatikana katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.
- Muhusika: maam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 11-12
- Imechapishwa: 18/05/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Kwanini Hizbiyyuun wameifumbia macho Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah?
Swali: Unasemaje juu ya mwenye kusema: “Ni lazima somo la ´Aqiydah leo lifupike na masuala ya kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah na uanasekula kwa sababu hayo ndio yameenea katika zama hizi. Ametumia hoja kwa Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ya kwamba ilikuwa inahusiana tu na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah kwa sababu ndio…
In "al-Fawzaan kuhusu sifa na alama za Ahl-ul-Bid´ah"

Kwanini Hizbiyyuun wameifumbia macho Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah?
https://www.youtube.com/watch?v=a7sqNy27XmU Swali: Unasemaje juu ya mwenye kusema: “Ni lazima somo la ´Aqiydah leo likomeke na masuala ya kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah na uanasekula kwa sababu hayo ndio yameenea katika zama hizi. Ametumia hoja kwa Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ya kwamba ilikuwa inahusiana tu na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah kwa sababu…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"
24. Maana halisi ya shirki na Radd juu ya tafsiri mbalimbali za kimakosa juu ya shirki
Kuko ambao wanaifasiri shirki kwamba ni kuabudu masanamu peke yake. Kuhusu kuwaabudu mawalii, makaburi, makuba na waja wema wanasema kwamba sio shirki. Wanaita hii kuwa ni Tawassul na kuomba uombezi na mfano wa hayo. Kwa mujibu wao wanaonelea kuwa shirki ni kule kuabudu masanamu peke yake. Tunawajibu kwa kusema kuabudu…
In "Sharh Nawaaqidh-il-Islaam - al-Fawzaan"