2- at-Twahaawiy (kfrk. 321) tabaka 11
adh-Dhahabiy ameandika wasifu wake katika ”Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:
”Imaam, ´Allaamah, Haafidhw na mtunzi wa vitabu vizuri Abu Ja´far Ahmad bin Muhammad bin Salaamah bin Salamah al-Azdiy al-Hijriy al-Miswriy at-Twahaawiy al-Hanafiy. Twahaa ni mji huko Misri.
Alisafiri kwenda Shaam mwaka wa 268 kwa ajili ya kusoma chini ya qaadhi Abu Khaazim na wengineo.
Ibn Yuunus amesema:
”Alizaliwa mwaka wa 237 na alikuwa mwaminifu, imara, Faqiyh na mwenye busara. Hakuacha baada yake mtu mfano wake.”
adh-Dhahabiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Abu Ja´far alitunga tofauti za wanachuoni, sharti, hukumu za Qur-aan na kitabu ”Ma´aaniy al-Aathaar”. Alikuwa ni mtoto wa dadake al-Muzaniy.
Ibn Yuunus amesema:
”Abu Ja´far alifariki mwanzoni mwa Dhul-Qa´dah mwaka wa 321, akiwa na zaidi ya miaka 80.”
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tadhkiyr-un-Naabihiyn, uk. 33-34
- Imechapishwa: 04/02/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)