41 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

تَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْ جَهْدِ البَلاءِ، وَدَرَكِ الشَّقَاءِ، وَسُوءِ القَضَاءِ، وَشَمَانَةِ الأَعْدَاءِ

“Ombeni kinga kwa Allaah kutokana na kuelemewa na mtihani, kuishilia kwenye naqama, mipango mibaya na furaha ya maadui.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

MAELEZO

Kuelemewa na mtihani bi maana uzito wa mtihani.

Kuishilia kwenye naqama bi maana mtu apatwe na taabu na hivyo akawa mla khasara.

Mipango mibaya bi maana akapangiwa mipango mibaya.

Furaha ya maadui bi maana maadui kufurahia yale matatizo yaliyompata.

Ni jambo limesuniwa kwa mtu kujilinda kutokana na mambo yote haya matatu. Kuomba kinga dhidi ya mambo haya ni jambo limesuniwa katika kila wakati. Ni mamoja ni katika Sujuud na kwenginepo.

[1] al-Bukhaariy (6616) na Muslim (2707).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 47
  • Imechapishwa: 12/10/2025