02 – Kumtakasia matendo Allaah pekee.

Inakupasa kuitakasa nia yako katika maneno na matendo. Kwani hakika matendo yote anayoyafanya mtu ni lazima yamtimizie nia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Amesema (Subhaanah):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende matendo mema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika hapana vyengine matendo huzingatiwa kwa nia.”[2]

[1] 18:110

[2] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 11
  • Imechapishwa: 27/01/2026