02. Hadiyth ”Je, Mtume alikuwa akiswali akiwa amevaa… ”

Imaam al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema: Aadam bin Abiy Iyaas ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia: Abu Maslamah Sa´iyd bin Yaziyd al-Azdiy ametukhabarisha:

”Nilimuuliza Anas bin Maalik: ”Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali akiwa amevaa viatu vyake?” Akasema: ”Ndio.”

Ameipokea al-Bukhaariy (386), Muslim (555), at-Tirmidhiy (1/310), ambaye amesema kuwa ni nzuri, Swahiyh na yenye kufanyiwa kazi na wanazuoni, an-Nasaa’iy (2/58), Ibn-ul-Jaaruud, uk. 68, Ahmad (3/100, 166 na 189), Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1/84), ad-Daarimiy (1/320), Ibn Sa´d (1/511) na al-Bayhaqiy (2/421).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 7
  • Imechapishwa: 27/05/2025