Hawa ndio waja Wake ambao adui yao hana mamlaka yoyote juu yao. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ
”Hakika waja wangu huna mamlaka nao.”[1]
Wakati adui wa Allaah Ibliys alipoona kuwa Allaah hamsalimishi mja Wake kwake wala hampatii uwezo juu yao, alisema:
فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
”Naapa kwa utukufu Wako kwamba nitawapotosha wote, isipokuwa wale waja Wako miongoni mwa wenye kutakasa nia!”[2]
Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ ۗ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ
”Hakika Ibliys alisadikisha dhana yake juu yao, basi wakamfuata isipokuwa kundi miongoni mwa waumini; lakini yeye hakuwa ana madaraka yoyote juu yao isipokuwa ili Tutambua ni nani yule anayeamini Aakhirah na nani yule anayeitilia shaka. Mola wako ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.”[3]
Hakumfanya adui Yake kuwa na uwezo juu ya waja Wake waumini, kwani wao wamo ndani ya hifadhi na ulinzi na usimamizi na wako chini ya uangalizi Wake. Hata kama adui Yake akamwinda mmoja wao kwa ghafla kama mwizi amwindavyo mtu aliyeghafilika, basi hili haliwezi kuepukika. Kwa sababu mja amejaribiwa na kughafilika, tamaa na hasira. Kuingia kwake adui huyu kwa mja ni kupitia milango hii mitatu. Hata mja akijitahadhari vipi, lazima apate kughafilika, lazima apate kutamani na ni lazima apate ghadhabu. Baba wa wanadamu, Aadam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alikuwa ni miongoni mwa viumbe wapole zaidi, wenye akili kubwa zaidi na waliothibitika zaidi. Pamoja na hayo adui wa Allaah hakumuacha mpaka akamfanya aanguke. Basi itakuwaje kuhusu mtu ambaye uvumilivu wake ni kama kipepeo na akili yake ikilinganishwa na akili ya baba yake ni kama mate ndani ya bahari?
Lakini adui wa Allaah hamfikii muumini isipokuwa kwa kumwinda kwa ghafla wakati wa kughafilika ambapo akamwangusha kisha akadhani kwamba hatamkabili tena Mola wake baada ya hayo na kwamba kuanguka huko kumemwangamiza kabisa. Lakini fadhilah ya Allaah, rehema Yake, msamaha Wake na kusamehe Kwake viko juu ya hayo yote. Basi anapotaka Allaah kheri kwa mja Wake basi humfungulia milango ya tawbah, kujutia, kunyenyekea, udhalilifu, kujihisi hana kitu, kutaka msaada kutoka Kwake, kuwa mkweli katika kumtegemea, kudumu katika kumnyenyekea na kumuomba na kumkaribia kwa mema yote anayoyaweza kiasi kwamba dhambi ile inakuwa ndiyo rehema juu yake. Mpaka adui wa Allaah aseme: “Laiti ningemwacha na sikumwangusha.” Hii ndiyo maana ya maneno ya baadhi ya Salaf:
“Hakika mja hufanya dhambi na kuingia kwa ajili yake Peponi na akafanya wema na akaingia kwa ajili yake Motoni.” Wakasema: ”Vipi hivyo?” Akajibu: ”Hufanya dhambi na haachi kuwa nayo mbele ya macho yake akiwa mwenye kuogopa, mwenye huzuni, mwenye kulia, mwenye majuto, mwenye haya kwa Mola wake, akiwa ameinamisha kichwa chake mbele Yake, moyo wake umevunjika kwa ajili Yake. Basi dhambi hiyo humfaidisha zaidi kuliko mema mengi kwa sababu ya mambo haya yaliyojitokeza baada yake ambayo ndani yake imo furaha ya mja na mafanikio yake, kiasi kwamba dhambi hiyo huwa ndiyo sababu ya kuingia kwayo Peponi. Upande wa pili hufanya wema, kisha haachi kujisifia nao mbele ya Mola wake, akajivuna nao, akajiona yeye ni bora, akavutiwa nao, akajitukuza nao na akaona kuwa amefanya mambo makubwa. Basi humpatia majivuno, kiburi, fakhari na kujikweza ambayo huwa sababu ya kuangamia kwake.”
Kwa hiyo Allaah akitaka kheri kwa mtu huyu masikini humjaribu kwa jambo linalomvunja na kumnyenyekesha na kumfanya ajione mdogo mbele Yake. Na kama hataki kheri kwake, humwacha pamoja na majivuno yake na kiburi chake, na hii ndiyo kutoswa na Allaah ambako husababisha maangamizi yake. Hakika wenye maarifa wote wamekubaliana kuwa tawfiyq ni kule Allaah (Ta´ala) kutokumuacha mja akajitegemea mwenyewe, kutoswa ni kule Allaah (Ta´ala) kukuacha ukajitegemea mwenyewe.
[1] 15:42
[2] 38:82-83
[3] ” 34:20-21
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 7-10
- Imechapishwa: 28/07/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 7-10
Imechapishwa: 28/07/2025
https://firqatunnajia.com/02-dhambi-ikampelekea-mtu-peponi-tendo-jema-likampelekea-mtu-motoni/