01. Ukimswalia Mtume mara moja, Allaah anakuswalia mara kumi

29 – ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]

Ameipokea Muslim.

30 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[2]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hizi mbili zinajulisha fadhilah za kumswalia Mtume wa Allaah kwa maana ya kwamba ambaye atamswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.

Maana bora iliyosemwa kuhusu Allaah kumswalia ni yale yaliyosemwa na Abul-´Aaliyah (Rahimahu Allaah):

“Allaah kumswalia Mtume wake ni kule kumsifu Kwake katika ulimwengu wa juu.”

Kwa hiyo unapomuomba Allaah amswalie kwa maana nyingine ni kwamba Amsifu katika ulimwengu wa juu, bi maana mbele ya Malaika.

[1] Muslim (384).

[2] Muslim (408).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 34
  • Imechapishwa: 07/10/2025