708- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuoga siku ya ijumaa kama akogavyo janaba halafu akaenda katika ile saa ya kwanza, basi ni kama ambaye amekurubisha ngamia. Mwenye kwenda katika ile saa ya pili ni kama ambaye amekurubisha ng´ombe. Mwenye kwenda katika ile saa ya tatu ni kama ambaye amekurubisha kondoo dume wa pembe. Mwenye kwenda katika ile saa ya nne ni kama ambaye amekurubisha kuku. Mwenye kwenda katika ile saa ya tano ni kama ambaye amekurubisha yai. Pindi imamu anapokuja wanahudhuria Malaika kuja kusikiliza ukumbusho.”[1]
Ameipokea Maalik, al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah. Katika al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Maajah imekuja:
“Inapokuwa siku ya ijumaa Malaika husimama kwenye mlango wa msikiti na kuandika wa mwanzo baada ya mwengine. Yule mwenye kuja mapema ni kama ambaye ametoa ngamia, halafu ni kama ambaye ametoa ng´ombe, kisha ni kama ambaye ametoa kondoo, kisha ni kama ambaye ametoa kuku halafu ni kama ambaye ametoa yai. Imamu anapokuja wanafunga madaftari yao ili wasikilize ukumbusho.”[2]
Ibn Khuzaymah amepokea mfano wake katika “as-Swahiyh” yake. Katika moja ya upokezi wake imekuja ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule mwenye kuja mapema ijumaa ni kama ambaye ngamia. Anayemfuatia ni kama ambaye ametoa ng´ombe. Anayemfuatia ni kama ambaye ametoa kondoo. Anayemfuatia ni kama ambaye ametoa ndege.”[3]
Katika [upokezi mwingine] imekuja:
“Katika kila mlango miongoni mwa milango ya misikiti siku ya ijumaa kuna Malaika wawili wanaoandika wa mwanzo baada ya mwengine. Mmoja ni kama ambaye amekurubisha ngamia, mwengine ni kama ambaye amekurubisha ng´ombe, mwengine ni kama ambaye amekurubisha kondoo, ambaye amekurubisha ndege, mwengine ni kama ambaye amekurubisha yai. Wakati imamu anapokaa wanafunga madaftari.”[4]
[1] Swahiyh.
[2] Swahiyh.
[3] Swahiyh.
[4] Swahiyh.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/443-444)
- Imechapishwa: 20/01/2018

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/443-444)
Imechapishwa: 20/01/2018
https://firqatunnajia.com/01-hadiyth-yule-mwenye-kuoga-siku-ya-ijumaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)