Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna siku ambazo matendo mema ndani yake yanapendeza zaidi na Allaah kuliko katika hizi siku kumi.” Wakasema: ”Hata jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Wala jihaad katika njia ya Allaah; isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake, kisha hakurudi na chochote kutoka humo.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ahmad.
Hadiyth hii ni dalili ya fadhilah za siku kumi za Dhul-Hijjah juu ya siku nyingine za mwaka, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshuhudia kuwa hizo ni bora kabisa katika masiku mengine ya dunia. Aidha amehimiza kufanya matendo mema ndani yake.
Vilevile ndani yake kuna dalili kuwa kila tendo jema ndani ya siku hizi ni lenye kupendeza zaidi na Allaah kuliko katika siku nyingine. Hii ni dalili ya fadhilah ya matendo mema ndani yake na wingi wa thawabu. Matendo yote mema huzidishwa katika siku hizi bila kubaguliwa kitu chochote.
[1] al-Bukhaariy (02/457), Abu Daawuud (07/103), at-Tirmidhiy (03/463), Ibn Maajah (01/550) na Ahmad (3/298). Tamko ni la at-Tirmidhiy.
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 5-6
- Imechapishwa: 04/05/2025
Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna siku ambazo matendo mema ndani yake yanapendeza zaidi na Allaah kuliko katika hizi siku kumi.” Wakasema: ”Hata jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Wala jihaad katika njia ya Allaah; isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake, kisha hakurudi na chochote kutoka humo.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ahmad.
Hadiyth hii ni dalili ya fadhilah za siku kumi za Dhul-Hijjah juu ya siku nyingine za mwaka, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshuhudia kuwa hizo ni bora kabisa katika masiku mengine ya dunia. Aidha amehimiza kufanya matendo mema ndani yake.
Vilevile ndani yake kuna dalili kuwa kila tendo jema ndani ya siku hizi ni lenye kupendeza zaidi na Allaah kuliko katika siku nyingine. Hii ni dalili ya fadhilah ya matendo mema ndani yake na wingi wa thawabu. Matendo yote mema huzidishwa katika siku hizi bila kubaguliwa kitu chochote.
[1] al-Bukhaariy (02/457), Abu Daawuud (07/103), at-Tirmidhiy (03/463), Ibn Maajah (01/550) na Ahmad (3/298). Tamko ni la at-Tirmidhiy.
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 5-6
Imechapishwa: 04/05/2025
https://firqatunnajia.com/01-fadhilah-za-masiku-kumi-ya-dhul-hijjah-na-matendo-mema-ndani-yake/