40 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa mara nyingi akiomba:

اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا في الدُّنْيَا حَسَنَةً، وفي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Ee Allaah, Mola Wetu! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na tukinge na adhabu ya Moto.”[1]

Kuna maafikiano juu yake.

MAELEZO

Du´aa hii ni miongoni mwa du´aa zilizokusanya. Ni du´aa tukufu ambayo imekusanya kheri za ulimwengu na za Aakhirah.

Mazuri ya dunia ni mke mwema, riziki nzuri na nyumba pana na mengineyo.

Mazuri ya Aakhirah ni kuokoka na Moto na kuingia Peponi.

Ambaye atapewa mazuri ya dunia na mema ya Aakhirah basi amepata kheri za ulimwengu na za Aakhirah na hivyo amepata kheri kubwa.

Du´aa hii ni miongoni mwa du´aa alizokuwa akiomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wingi. Kwa hivyo inatakiwa kuifanya ndio hitimisho katika kuomba. Muislamu anatakiwa kuwa na hima kubwa na hivyo amwombe Allaah mema ya dunia na ya Aakhirah. Akithirishe du´aa hii, kwani ni du´aa kubwa. Du´aa hii imekuja kwa njia tatu:

1 –

رَبَّنَا آتِنَا في الدُّنْيَا حَسَنَةً، وفي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Ee Mola Wetu! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na tukinge na adhabu ya Moto.”

Kama ilivyokuja katika Aayah. Ameipokea Muslim.

2 –

اللهم آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Ee Allaah! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na tukinge na adhabu ya Moto.”

Kama ilivyokuja kwa Muslim.

3 –

اللَّهُمَّ رَبَّنَا آتِنَا في الدُّنْيَا حَسَنَةً، وفي الآخِرَةِ حَسَنَةً، وقِنَا عَذَابَ النَّارِ

“Ee Allaah, Mola Wetu! Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na tukinge na adhabu ya Moto.”

Unakusanya kati ya “Ee Allaah” na “Ee Mola wetu”, kama ilivyokuja kwa al-Bukhaariy na Muslim wote wawili.

[1] al-Bukhaariy (6389) na Muslim (2690).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 12/10/2025