Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wana maadui ambao wanawazuia watu na lingano zao. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا
“Hivyo ndivyo Tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu; na Mola wako anatosheleza kuwa ni Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.” (25:31)
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ
”Namna hiyo ndivyo Tulivyofanya kwa kila Nabii maadui mashaytwaan wa kiwatu na kijini – wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya kudanganya. Lau angetaka Mola wako wasingeliyafanya hayo; basi waachilie mbali na wanayoyazusha. Na ili zielemee katika [udanganyifu] nyoyo za wale ambao hawaamini Aakhirah na ili waridhike nayo na ili wachume [madhambi] wanayoyachuma. Je, nitafute hakimu asiye Allaah na hali Yeye ndiye aliyekuteremshieni Kitabu kilichopambanua waziwazi? Hakika wale Tuliowapa Kitabu kabla wanajua kuwa kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Basi usije kuwa miongoni mwa wanaotia shaka.” (06:112-114)
Hii ndio mwenendo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa viumbe Wake. Kila anapojitokeza mlinganizi anayelingania katika haki, basi anakabiliwa na walinganizi wa upotevu. Lakini pamoja na hivyo siku zote haki inashika njia yake na kubaki. Ama kuhusu walinganizi wa upotevu athari yao inakatika na mambo yao yanakwisha:
فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً ۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ َۚ
“Basi povu linapita kama takataka, lakini vile vinavyowafaa watu hubakia ardhini.” (13:17)
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 10-11
- Imechapishwa: 07/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 10-11
Imechapishwa: 07/02/2026
https://firqatunnajia.com/01-batili-inapokutana-na-haki/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket