1 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anasema: “Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania na Mimi ni pamoja Naye anaponitaja.”[1]

MAELEZO

Maana ya Hadiyth al-Qudsiy ni kwamba tamko na maana yake ni kutoka kwa Allaah. Lakini inatofautiana katika maana, na si kama ilivyo katika utambulisho ulioshuhurika ambao unaenda sambamba na ´Aqiydah ya Ashaa´irah ya kwamba maana yake ndio yenye kutoka kwa Allaah. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania… ”

Hapa inafahamisha kuwa mja anatakiwa kumdhania Allaah vyema na sambamba na hilo afanye matendo mema. Kwa sababu anayefanya matendo mema, dhana yake itakuwa njema, na anayefanya matendo maovu, dhana yake itakuwa mbaya. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na Mimi ni pamoja Naye anaponitaja.”

Hapa inafahamisha kuwa ni upamoja wa Allaah pamoja na wale wenye kumtaja, jambo ambalo linapelekea kuwawafikisha, kuwatia nguvu, kuwahifadhi na kuwalinda. Kuna upamoja wenye kuenea kwa waumini na kwa makafiri. Huo ni ule upamoja wa Yeye kuwaona, kuwasikia na kuwafanya anachotaka.

[1] al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 07
  • Imechapishwa: 23/09/2025