Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake, Maswahabah zake wote na wale wote watakaowafuata mpaka siku ya Qiyaamah.

Ama baada ya hayo;

Miongoni mwa vitu bora ambavo mja anaweza kujishughulisha navyo ni kumtaja Allaah, kama alivosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah[1]. Wanazuoni wamekusanya du´aa na adhkaar zinazosemwa na mtu anapoamka asubuhi, anapofika jioni, anapoogopa kitu na mfano wa sababu kama hizo. Mwenye kushika njia hiyo, basi ameshika njia ya mawalii wa Allaah ambao hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

Huu ni mukhtaswari wenye faida wa du´aa na adhkaar. Sambamba na hilo nimebainisha maana yake kwa kufupisha katika yale yaliyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim (Rahimahumaa Allaah) katika “as-Swahiyh” zao. Nimezitoa humo na nikaweka chini yake milango ya fadhilah za kumtaja Allaah, fadhilah za adhkaar maalum, sehemu za kuitikiwa du´aa, adhkaar zilizoachiwa na zilizofungamanishwa. Nimeweka wazi baadhi ya maana yake kwa ajili ya kujikumbusha mwenyewe na ndugu zangu waislamu kwa kutaraji Allaah kuwanufaisha nazo.

Nimamuomba Allaah anufaishe kwacho, ndugu zangu waislamu kwa yale tunayoyasema na kuyatenda, afanye kitendo hichi kiwe kwa ajili ya uso Wake mtukufu na atuthbitishe sote juu ya dini na njia Yake ilionyooka. Kwani hakika Yeye ndiye Mwenye jukumu ya hilo, mbora wa kuombwa.

Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake, Maswahabah zake wote na wale wote watakaowafuata mpaka siku ya Qiyaamah.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/660).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 05-06
  • Imechapishwa: 23/09/2025