Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu, ambaye amemtuma Mtume Wake kwa uongofu na dini ya haki ili iweze kuwa juu ya dini zingine zote hata kama washirikina watachukia. Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad aliyesema:
“Allaah hutuma kwa ajili ya ummah huu mwanzoni mwa kila mwaka mtu mwenye kuifanya upa dini yake.”[1]
Allaah amejaalia katika kila kipindi miongoni mwa zama kuwepo kwa wanazuoni wanaolingania katika Qur-aan, kuwafunza nayo watu, kumlingania mwenye kupotea katika uongofu na kueneza kheri. Hilo linathibitisha ukweli wa maneno Yake (Ta´ala):
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
“Hakika Sisi tumeteremsha Ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio tutakaoihifadhi.” (15:09)
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakitoacha kikundi katika ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hawatowadhuru wale wenye kuwakosesha nusura wala na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”2
Miongoni mwa maimamu hawa wenye kuhuisha dini ni Shaykh, Imaam, ´Allaamah, Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Mtu huyu alisimama kuifanya upya dini hii katika nchi hii na kufanya kwake upya kukaenea mpaka nje ya mji huu. Kila elimu yenye manufaa na kila mwalimu ambaye nia yake imetakasika, basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huweka athari nzuri juu ya ummah vyovyote maadui watavyosimama dhidi yake. Hakuna namna ya kuficha jua katika mchana kweupe. Yote waliyofanya na kuyasema dhidi ya mwanachuoni huyu na dhidi ya ulingano wake, Allaah ni mwenye kuinusuru dini Yake na kuidhihirisha haki juu ya batili. Haijalishi kitu yule atayechukia hilo. Hii ni Sunnah ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa waja Wake ya kwamba anawapa mtihani na majaribio kwa walinganizi wapotevu ambao wanasimama kidete katika kukabiliana na haki na watu wa haki. Lakini hata hivyo mwisho mwema siku zote unakuwa kwa watu wa haki. Upande mwingine adhabu inakuwa kwa watu wa batili.
[1] Abu Daawuud (4291), al-Haakim (04/522), Taariykh (02/61-62) ya al-Khatwiyb al-Baghdaadiy.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 7-10
- Imechapishwa: 07/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Radd Shubuhaat hawl Da´wat-il-Mujaddid, uk. 7-10
Imechapishwa: 07/02/2026
https://firqatunnajia.com/00-namna-maadui-walivyosimama-dhidi-ya-ibn-abdil-wahhaab/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket