Tasmiyah na Isti´aadhah vinaletwa kisirisiri katika Tarawiyh


Swali: Nimeona kuwa baadhi ya maimamu katikati ya swalah ya Tarawiyh au wakati wanapokuwa wamesimama mwanzoni mwa Suurah wanaleta Basmalah kwa sauti na wengine hawaleti Basmalah kwa sauti. Ni ipi hukumu ya kitendo chao hichi? Je, hukumu inatofautiana ikiwa swalah ni ya faradhi au ya sunnah?

Jibu: Sunnah ni kuleta Isti´aadhah na Tasmiyah kisirisiri katika swalah za kusoma kwa sauti. Ni mamoja ikawa ni swalah ya faradhi au ya sunnah. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Niliswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar na walikuwa wakileta “Bismillaah ar-Rahmaan ar-Rahiym” kisirisiri.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Sikumsikia yeyote katika wao akisoma “Bismillaah ar-Rahmaan ar-Rahiym.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (244), an-Nasaa´iy (908) na Ibn Maajah (815).

[2] al-Bukhaariy (743), Muslim (399), at-Tirmidhiy (246), an-Nasaa´iy (907), Abu Daawuud (782) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/27)
  • Imechapishwa: 21/05/2018