Muislamu kumpa amani kafiri kwa kumwingiza katika nchi ya Kiislamu

Swali: Mmoja katika Waislamu akimpa amani kafiri pasina idhini ya mtawala…

Jibu: Hakuna neno hata kama mtawala hakutoa idhini. Mtawala anakubali hili.

Swali: Je, mtawala anaweza kumuua kafiri huyu akiona kuna maslahi?

Jibu: Hapana. Haijuzu kwa yeyote kumuua maadamu hakujaonekana kitu kinachowajibisha kuuawa. Maadamu hakujapitika kwake kinachowajibisha kuuawa haijuzu kumfanyia uadui. Akifanya kitu kinachowajibisha kuuawa, anayetakiwa kumuua ni mtawala na si mtu ni mtu tu akamuua. Dini sio vurugu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-06-05.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014