Mtu ajisafishe vipi akiwa na maji madogo tu?

Swali: Je, nioge kwa maji madogo sehemu iliyopatwa na janaba au nifanye tu Tayammum pasi na kuosha dhakari pindi mikipatwa na janaba na sina maji isipokuwa madogo tu?

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa mwenye janaba akipata maji madogo yasiyomtosheleza, basi ni wajibu kwake kujisafisha nayo sehemu ya siri na kutawadha. Halafu baada ya hapo afanye Tayammum kwa udongo. Ajisafishe kwa maji haya kwa njia ya kwamba aoshe dhakari yake na pembezoni mwake. Kisha asukutue kinywa chake na aoshe uso wake, mikono yake, kichwa chake na miguu yake. Kukibaki kitu basi aoshe sehemu ya mwili wake kisha afanye Tayammum sehemu itayokuwa imebaki. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Afanye kile anachoweza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 21/02/2019